Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete
akimpongeza Bw. Deo Mwanyika, Makamu wa Rais wa Kampuni ya Barrick
Tanzania baada ya kuibuka mchangiaji mkubwa kwa kutoa dola za Kimarekani
laki 5 kwa ajili ya kuchangia taasisi ya Mkapa Hiv/Aids Foundation
Jumanne Juni 5, 2012 usiku katika hoteli ya Kilimanjaro jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan
Mwinyi na kulia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mzee Benjamin William
Mkapa aliyeandaa hafla hiyo iliyoweza kukusanya shilingi bilioni 3.2 na
kuvuka malengo ya harambee hiyo kwa asilimia sita.
Rais Jakaya Kikwete, akimkabidhi
picha ya kuchora Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya UNDI Consulting Group
Limited, Bw Philip Makoka aliyoinunua kwa shilingi milioni 20 wakati wa
Harambee ya kuchangia fedha programu ya Mkapa Fellows inayoendeshwa
naTaasisi ya Mkapa HIV/AIDS iliyofanyika Dar es Salaam kwenye hoteli ya
Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. Kulia ni mchoraji wa
picha hiyo, Bwana Muzu.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete
akisindikizwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi
(kushoto) na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Mzee Benjamin William Mkapa
baada ya kuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia Taasisi ya Mkapa
HIV/AIDS foundation na kusaidia kukusanya shilingi bilioni 3.2 na kuvuka
malengo ya harambee hiyo kwa asilimia sita.
(PICHA NA IKULU)
No comments:
Post a Comment