KAMPUNI ya Bia Tanzania
(TBL), leo imekabidhi hundi ya Sh. Milioni 20 kwa klabu ya Simba SC ya Dar es
Salaam, kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa klabu hiyo, unaotarajiwa kufanyika Agosti
5, mwaka huu kwenye ukumbi wa Polisi Oysterbay, Dar es Salaam.
Akikabidhi mfano wa
hundi hiyo kwa Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geofffrey Nyange ‘Kaburu’, Meneja
wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, inayozalishwa na TBL, George Kavishe
alisema kwamba anawatakia mafanikio Simba SC katika mkutano wao huo Mkuu.
Kwa upande wake, Kaburu
au Perez ambaye klabu yake, inadhaminiwa na Kilimanjaro Beer, alisema kwamba anashukuru
kwa fedha hizo na akawataka wanachama wote hai wa Simba kuhudhuria mkutano huo
siku hiyo kujadili maendeleo ya klabu.
Kaburu alisema kwamba,
katika siku hiyo ya Mkutano watazindua Wiki ya Simba SC na jamii, ambayo itahusu
wachezaji, viongozi na walimu wa timu hiyo kufanya ziara sehemu mbalimbali za
kijamii, kama hospitali, vituo vya watoto wa yatima, shule za msingi na kiwanda
cha TBL, wadhamini wao wakuu.
Kaburu pia alikumbushia
kuhusu tamasha la kila mwaka la Simba SC, Simba Day, ambalo na mwaka huu tena
litafanyika Agosti 8, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. “Maandalizi ya Simba Day
yamekwishaanza na yanaendelea vizuri na kwa sasa kocha yupo kwenye harakati za
kuboresha timu,”alisema Kaburu.
Kwa upande wake, Kavishe
aliahidi siku ya Simba Day wataikabidhi Simba SC basi lake jipya kubwa, ambalo
kwa sasa lipo kwenye hatua za mwishoni za matengenezo.
![]() |
Kaburu kushoto, kulia Kavishe wakizungumza leo TBL, Ilala |
RATIBA YA WIKI YA SIMBA NA JAMII:
Agosti 5, 2012: Mkutano Mkuu wa mwaka Simba SC (Polisi Oystrebay)
Agosti 6, 2012: Kutembelea watoto yatima Maungu Orphanage Center, K’ndoni
Mkwajuni
Agosti 7, 2012: Kutembelea wagonjwa Mwananyamala hospitali
Agosti 8, 2012: Simba Day (Uwanja wa Taifa, burudani na mechi)
Agosti 9, 2012: Kutembelea shule ya msingi Mgulani kuhamasisha
michezo mashuleni
Agosti 10, 2012: Kutembelea kiwanda cha TBL Ilala
No comments:
Post a Comment