LONDON, England
KOCHA wa Arsenal, aliyekuwa akisuasua kumuuza Robin van Persie kwenda Manchester United amekubali kwa dau la Pauni 23 milioni.
KOCHA wa Arsenal, aliyekuwa akisuasua kumuuza Robin van Persie kwenda Manchester United amekubali kwa dau la Pauni 23 milioni.
Arsenal ilithibitisha kukamilika kwa 'dili' hilo na mchezaji huyo amekwenda Manchester kwa ajili ya kufanyiwa vipimo.
Klabu
hiyo ilikubalia kuanzishwa upya kwa mazungumzo, na lengo ni kumchukua
mchezaji huyo na sas Van Persie ni mchezaji halali wa United.
Alex Ferguson alisema, kumsajili mchezaji huyo, sasa itakuwa kazi kwa Manchester City kutetea taji lake.
Wenger alifanya kazi ya ziada kumshawishi Van Persie kubakia lakini ilishindikana na Van Persie alikuwa anataka kuondoka tu.
Wenger alifanya kazi ya ziada kumshawishi Van Persie kubakia lakini ilishindikana na Van Persie alikuwa anataka kuondoka tu.
Kocha
huyo wa Arsenal aliulizwa na Televisheni ya Ufaransa kama alikuwa na
mpango wa kununua mchezaji mwingine: "Tayari tumeshanunua mchezaji, yuko
[Lukas] Podolski na [Olivier] Giroud. Tunasikitika kumpoteza mchezaji
mwenye ubora, lakini mkataba wake umebakia mwaka mmoja na hatuna jinsi."
Van
Persie aliweka wazi katika taarifa yake ya Julai 4 kwamba anataka
kutwaa mataji. Kwa njia nyingine, hafurahishwi na jinsi Arsenal FC
inavyokwenda". Alikataa moja kwa moja kumwaga wino na alikuwa amebakiwa
na miezi 12. Arsenal ilikuwa ikimtaka kwa udi na uvumba mchezaji huyo.
Taarifa
ya Arsenal ilisema: "[Sisi] kama Arsenal tunathibitisha Robin van
Persie amekwenda Manchester United. Van Persie anakwenda Manchester kwa
ajili ya kufanyiwa vipimo kabla ya kuanza mazoezi."
Arsenal
ilitangaza Paundi 20 milioni kama bei ya kumuuza mchezaji huyo. Kabla ya
kwenda nchi za Asia Julai 21, ambako Van Persie hakwenda na klabu
ilipokea ofa kutoka klabu za United, City na Juventus, ambazo zote
zilimtaka kwa Paundi 15 milioni.
Juzi United iliandika kwenye
mtandao wake kuwa "Taarifa Mtu aliyekuwa na furaha alikuwa Wayne Rooney,
ambaye alisema sasa safu yao ya ushambuliaji imekamilika.
"Van
Persie ni mkali," Rooney alisema. "Amefanya makubwa akiwa na Arsenal kwa
miaka mingi. Kuja kwake kutaongeza thamani ya timu na sasa itakuwa Rom +
Roo."

No comments:
Post a Comment