SERIKALI imetakiwa kuangalia upya gharama za uingizaji mitambo
mbalimbali ikiwamo ya kuchimba visima, ili kuwezesha wananchi kupata
huduma ya maji kwa urahisi.
Akitoa taarifa ya Taasisi ya Rehema Friendship Trust kwa Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal, Mwakilishi wa Taasisi hiyo , Abdi Adam alisema gharama ya kuchimba visima viwili au vitatu kwa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, inachimba kisima kimoja kwa Mkoa wa Shinyanga.
Alisema baada ya kurejea masomoni kutoka nchini Uturuki, aliomba taasisi hiyo kumwachia bajeti ya mwaka huu ili kupeleka mrejesho nyumbani kwao Wilaya ya Kishapu, Shinyanga lakini gharama za kuhamisha mitambo zimekuwa kubwa.
“Tunaomba Serikali kuangalia suala la gharama hizi zimekuwa kubwa, hivyo wahisani wanashindwa kuzimudu hatua ambayo inasababisha wananchi kukosa huduma muhimu kama maji,” alisema Adam kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na taasisi hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Alisema taasisi hiyo tayari imechimba visima 40 sehemu mbalimbali zenye mahitaji, imesaidia zaidi ya watoto yatima 400 na kwamba, hivi sasa inatarajia kuboresha makazi ya watoto hao.
“Tunaamini taasisi nyingine zinafanya zaidi ya hapo lakini hata sisi tunajaribu pale ambako panawezekana,” alisema Adam. Rehema ilianzishwa na baadhi ya Watanzania na Waturuki wanaoishi nchini.
Awali, Mwenyekiti wa Rehema, Muhammed Karabacar alisema taasisi hiyo siyo ya kidini bali inashirikiana na dini zote kuhakikisha ustawi wa Mtanzania unaendelea.
“Kwa sababu tunaamini dini zinajenga amani tunayojivunia nayo duniani, tunashirikiana na dini zote kuhakikisha tunaimarisha ustawi wa Mtanzania na nchi inaendelea kuwa kisiwa cha amani,” alisema Karabacar.
Baadhi ya viongozi wengine maarufu walioshiriki futari hiyo ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, Sheikh Mkuu wa Tanzania, Issa Shaaban bin Simba, Kadhi Mkuu aliyeteuliwa hivi karibuni na Bakwata, Abdallah Mnyasi, Sheikh Ali Basaleh na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa.

No comments:
Post a Comment