Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imerudisha utaratibu wa mihula kama
ilivyokuwa zamani kutokana na kile ilichoeleza kuwa utaratibu wa sasa
unasababisha walimu kutumia muda mwingi kusimamia na kusahihisha
mitihani wakati wa masomo.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo amesema kwamba mwakani utaratibu wa kufanya mitihani kwa Kidato cha Nne na wa Kidato cha Sita utakuwa kama ilivyokuwa zamani.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo amesema kwamba mwakani utaratibu wa kufanya mitihani kwa Kidato cha Nne na wa Kidato cha Sita utakuwa kama ilivyokuwa zamani.
- Wakati hivi sasa mitihani ya Kidato cha Nne imekuwa ikifanyika Oktoba, mwakani itafanyika Septemba.
- Kwa upande wa Kidato cha Sita ambao mitihani imekuwa ikifanyika Februari, mwakani itakuwa Mei.
- Utaratibu wa likizo utaendelea kuwa Juni na Desemba.
“Mwakani tunarudi kama ilivyokuwa mihula ya zamani. Kidato cha Nne wafanye mitihani Novemba badala Oktoba na Kidato cha Sita itakuwa mitihani Mei kama zamani ili walimu wabaki kufundisha shuleni badala ya kuzunguka kwenye mitihani na kusimamia,” alisema Naibu Waziri.
Uamuzi huo unalenga kuondoa kile ambacho baadhi ya wabunge walilalamikia kuwa baadhi ya walimu wamekuwa badala ya kufundisha, kutumia muda mwingi kusimamia mitihani na pia kwenda kusahihisha.
Kwa utaratibu uliorejeshwa, usahihishaji kwa Kidato cha Sita utafanyika kipindi ambacho wanafunzi watakuwa likizo ambacho ni Juni.
Vivyo hivyo kwa Kidato cha Nne baada ya mtihani utakaofanyika Novemba, usahihishaji utafanyika Desemba.
HabariLeo
No comments:
Post a Comment