WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda, ameitaka Tume ya Ushindani nchini (FCC), kuhakikisha inalimaliza haraka tatizo la bidhaa bandia zilizozagaa mitaani kwani ni aibu kwa serikali.
Dk. Kigoda alitoa agizo hilo jana alipofanya ziara ya kufahamiana na wafanyakazi wa tume hiyo pamoja na Baraza la Ushindani (FCT).Katika ziara hiyo ambayo aliambatana na naibu wake, Gregory Theu, alisema jamii imekuwa ikiitupia lawama serikali kuhusu bidhaa hizo kutokana na tume hiyo iliyokabidhiwa jukumu kutojulikana kazi zake kwa jamii.
“Huko mitaani kuna taarifa nyingi kuhusu bidhaa bandia na hafifu ambapo wananchi hawaelewi ni nani anawajibika katika udhibiti wake, hivyo wizara kusukumiwa lawama. Jitangazeni kwa gharama ndogo kupitia vyombo vya habari, jamii iwatambue,” alisema.
Kwa upande wa FCT, Kigoda alitoa wito kwa watendaji kuwa wabunifu katika kutafuta njia zitakazowafanya watambulike katika jamii.
No comments:
Post a Comment