MWIGIZAJI wa filamu wa kiume Eliya Daniel 'EllyG'anatarajia kuziba pengo la msanii nyota marehemu, Steven Kanumba aliyefariki dunia Aprili mwaka huu. Msanii huyo amesema baada ya kifo cha Kanumba alitumia muda mwingi katika kujifua na kuamua kuanza kutayarisha filamu zake kama alivyokuwa akifanya Kanumba na amefanikiwa kwa sasa anamalizia filamu yake inayoitwa Malaika shetani.
Eliya Daniel 'Elly G'
"Kabla ya Kanumba kufariki dunia, wapenzi wa filamu walikuwa wakinifananisha na Kanumba kwa mwonekano hata uigizaji kwa kuguswa na hilo nimedhamilia kuziba pengo lake kwa kutafuta fursa mbalimbali katika tasnia ya filamu ikiwa na kufungua kampuni yangu kwa ajili ya utengenezaji wa filamu," anasema Elly G. Msanii huyo amedai kuwa katika kumuenzi Kanumba tayari amefungua kampuni inayojulikana kwa jina la Vita Production ambayo inarekodi filamu zake pamoja na kazi za wasanii wengine, huku akijiandaa kwa ajili ya kwenda nje Nchi kwa ajili ya kutangaza tasnia ya filamu kama alivyokuwa Kanumba.
No comments:
Post a Comment