LAGOS, NIGERIA
NDOA nyingi za wasanii wa kike wa Nollywood zimesambaratika kwenye mazingira ya kutatanisha huku sababu kubwa ikielezwa kuwa ni kuendekeza kwao starehe na kutojali, ingawa wenyewe wanadai wamekimbia mateso.
Mchambuzi wa filamu za Nollywood amegusia ndoa kumi zilizosambaratika miaka ya hivi karibuni, hebu soma habari zake.
KateHenshaw:Nilikumbwana migogoro ya ndani ya familia. Uhusiano wangu ulivunjika ndani ya miaka minne, nilikuwa sijitambui. Nilijikuta sitabasamu wala kucheka, lakini nilikuwa na ujasiri wa kusimama imara na kurejea kwenye hali yangu ya kawaida. "Nilikuwa nalazimisha mabadiliko kwa vile yule mwanamume aliniumiza sana, alikuwa ananipiga tukiwa ndani hata akinikuta kwenye sehemu niko na watu. "Kuna kipindi nilikuwa nimefungwa plasta gumu mguuni na mliniona nikitembea nalo, ilikuwa ni kwa sababu yake."Mbali ya yote hayo, alikuwa anasema ananipenda na anataka kunioa na nilishanunua mpaka vifaa vingi vya ndani na nilikuwa tayari kuzaa naye, lakini uvumilivu ulinishinda. "Nilikuwa nona aibu kusema mbele ya jamii wakati huo, alinivunja enka."Hayo yote ni maneno ya msanii huyo ambaye sasa ameolewa na mzungu na wana mtoto mmoja.
Monalisa Chinda:Baada ya miaka mingi ya kuvumilia vipigo, aliamua kuachana na mumewe mwaka 2009 wakiwa wamedumu katika ndoa kwa miaka mitano tu. "Ndoa yangu haikuwa ya kawaida, nitakuwa mjinga kama nisipokiri kwamba matatizo yalikuwa mengi mno. Kuna kipindi nilikuwa nafanya mambo yangu kama chizi, nilichanganyikiwa," anasema. "Nilivumilia miaka mitano nikajua mambo yataenda sawa, lakini ikashindikana, nilikuwa naendelea kufa kidogo kidogo. Nilizidiwa ilikuwa Julai 10,2009 nikaamua kuondoka kurudi kwetu." Tangu wakati huo Monalisa hajaolewa tena, lakini mara kwa mara amekuwa akionekana viwanja usiku akitanua na jamaa mmoja.
Vivian Ejike:Ni mzuri. Lakini hiyo haikumsaidia kuepuka vipigo kwa mumewe. Ni prodyuza wa filamu zikiwamo 'Private Storm' na 'Silent Scandal'. Aliachana na jamaa yake baada ugomvi wa kipindi kirefu. "Nilikuwa nimeolewa, lakini nikaamua kutoka kwa vile shida zilizidi, nilikuwa sina raha. Hata filamu yangu ya Private Storm niliitengeneza kwa sababu ya hayo maneno yaliyokuwa yananisumbua. Lakini nashukuru kwamba nimeolewa tena na naishi kwa amani sasa," anasema msanii huyo msomi.
Ayo Adesanya :Ni msanii anayevuka mipaka sana na kufanya biashara zake kila kona ya Afrika na Ulaya. Aliachana na prodyuza wa filamu za Nollywood ambaye aliishi naye miaka minane. "Nilifungasha nikaondoka usiku wa manane, sidhani kama mtu anatakiwa kuendelea kukaa kwenye uhusiano wenye matatizo kila kukicha," anasema.
Zaaki Azzay Hadiza:"Alinitoa damu zaidi ya mara mbili kutokana na kipigo, nilikuwa nifie mikononi mwake. Niliondoka kwake mara nyingi sana kutokana na kudhalilishwa, nilienda kwetu kama mara nane hivi. Mwishowe nikaona haina haja kuendelea naye."
Fathia Balogun:Alikaa na jamaa yake miaka minne tu wakaachana baada ya mambo kuzidi kuwa magumu. Kila mmoja alieleza kutokuwa na imani na mwenzake, ilifikia hatua mbaya mumewe alivyomchapa vibao mtaani siku moja akiwa na mashoga zake.
Chika Ike:Walioana kimkataba mwaka 2006 na mumewe, lakini baada ya miaka miwili mambo yakabadilika kila mtu akachukua njia yake. Alikuwa anaonekana na makovu mara kwa mara lakini akawa anaficha na kutoiambia jamii kilichokuwa kinaendelea. Maji yalipozidi unga ikabidi aondoke mwenyewe kutunza heshima, ingawa marafiki zake walivujisha siri.
Kefee:Aliolewa kwa mbwembwe mwaka 2006 lakini baada ya miaka miwili akaachana na mumewe. Lakini ameshaweka mambo sawa na kuanza uhusiano mpya.
Katherine Edoho:Alizoea kunipiga, lakini kipigo cha mwisho kilikuwa ni habari nyingine kabisa. Nilikuwa nazuia macho yangu, jamaa alikuwa ananipiga kama anapiga mwanamume mwenzake. "Ilikuwa hatari sana kwangu. Nililazimika kuvaa miwani kuficha aibu na nikakaa Cameroon kwa muda."
Foluke Daramola:Foluke Daramola, alishindwa kuvumilia akarudi kwao kutokana na hasira. Aliishi na jamaa yake kwa miaka minne, ametoa filamu kali kama 'Omo Britiko', 'Jeun Soke', 'Agogo Eewo', 'Ayo Mi Da', 'Omoge Campus', 'Ale Ariwo', 'Duro Dola' na 'Ife Ti Tan'.
No comments:
Post a Comment