Habari ya Mjini.
Na Musa Mateja
MSANII wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Estelina Sanga ‘Linah’, amekuja juu akijibu madai kwamba, aliwahi kufa na kufufuliwa na Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kwa kumfanyia maombi.
Akizungumza na gazeti hili, Oktoba 2, mwaka huu, Dar es Salaam, Linah alisema hajawahi kukumbwa na tukio hilo zaidi ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kuzimia mara kwa mara na kuponywa kwa njia ya maombi na Gwajima.“Kwenye maisha yangu sijawahi kufa na kufufuka, kama umesikia hivyo basi hayo yalikuwa ni maneno tu, hapo mwanzo nilikuwa na kitu kama masheteni yalikuwa yakinikaba na kunifanya nipoteze fahamu mpaka nilipoombewa na Gwajima,” alisema Linah.
No comments:
Post a Comment