Picha ya chini hapa mkurugenzi wa Perfect Classic Salon (kati mwenye nguo nyeusi) Bi. Ester Kiama akitoa maelekezo kwa mmoja ya wafanyakazi wa Salon yake jinsi ya kumtengeneza mshiriki wa Epiq Bongo Star Search (EBSS 2012). Perfect Classic Salon imedhamini shindano hilo kwa kuwapendezesha washiriki na kuwapa muonekano mpya wanapokuwa wakiimba stejini.
Wafanyakazi wa Perfect Classic Salon wakiwasuka na kuwapamba washiriki wa Epiq Bongo Star Search 2012 katika jumba lao lililopo jijini Dar.
Perfect Lady Salon yadhamini shindano la Epiq Bongo Star Search 2012 kwa kuwapamba na kuwapa muonekano mpya washiriki wote walio katika kinyanga’anyiro hicho.
Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa kuwatambulisha wadhamini uliofanyika wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, mkurugenzi wa Perfect Lady Salon Bi. Ester Kiama alisema kuwa ikiwa yeye ni mtanzania anayependa maendeleo ya vijana ameona ni vyema kujitoa kudhamini shindano hilo kwa kuwapa washiriki muonekano mpya.
“Nafurahi sana kuungana na Bi. Ritta Poulsen kudhamini shindano hili linalovumbua vipaji vya vijana ambapo mimi, nimechukua upande wa kuwapamba washiriki na kuwapa muonekano mpya wawapo stejini,” alisema Ester Kiama.
Hata hivyo aliongeza kuwa wakati umefika kwa Watanzania kuungana mkono pale unapoona mtu anafanya jambo linaloleta maendeleo katika nchi yetu.
Pia Bi. Ester Kiama alisema, Perfect Lady Salon imefungua milango kwa mtu yeyote ambaye anahitaji kufanya kazi na nao, asisite kuwasiliana nao wanapatikana Kinondoni mkabala na Chuo Kikuu Huria.
Shindano la EBBS linaendelea ndani ya Stesheni ya ITV na sasa wapo katika hatua ya mtoano.
No comments:
Post a Comment