WAWATISHIA MAISHA WAANDISHI
MABINGWA wa soka Afrika Mashariki na Kati, Yanga ya jijini Dar es Salaam leo inatarajiwa kushuka kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza kuwavaa wenyeji Toto African katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom.Yanga itashuka uwanjani ikiwa bado na maumivu ya kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar ya Kagera mjini Bukoba Jumatatu.Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrance Mwalusako, alisema jijini Dar es Salaam jana kwamba, baada ya kipigo cha Kagera, wamefanyia kazi upungufu uliojitokeza na anaamini watashinda leo.Alisema zaidi ya kuwaweka sawa wachezaji kwa ajili ya mchezo huo, pia wamewajenga kisaikolojia ili waweze kusahau ya Kagera na kuelekeza nguvu katika michezo mingine ya ligi hiyo.
“Mchezo ni mchezo lazima kuwepo na upinzani, hivyo nasema utakuwa ni mgumu…kikubwa ni kuwa tumejipanga katika kila idara kuhakikisha tunaondoka na pointi tatu,” alisema.
Katika mchezo wa leo, Yanga itawakosa nyota wake muhimu wakiwemo beki Kelvin Yondani pamoja na Said Bahanuzi ambao ni majeruhi.Yanga hivi sasa inakamata nafasi ya nane katika msimamo wa ligi, ikiwa na pointi 8 baada ya kushuka dimbani mara sita.Katika tukio jingine, wanachama wa Yanga, maarufu kama makomandoo wametishia maisha mwandishi wa habari za michezo wa Kampuni ya New Habari Corporation, Onesmo Kapinga kwa madai ya kuandika habari kuwa wachezaji wa timu hiyo walipokuwa Bukoba walilala wawili wawili chumba kimoja.
Vitisho hivyo vimetolewa jijini Mwanza juzi, baada ya habari hiyo kuandikwa na moja ya magazeti ya kampuni hiyo, jambo lililowaghadhabisha makomandoo hao na kuamua kutangaza kumdhuru mwandishi huyo.
Mbali na Kapinga, pia yupo mwandishi wa Nipashe, Somoe Ng’itu ambaye pia ametangaziwa ‘kutiwa adabu’ na kundi hilo, kwa madai amekwenda Bukoba kwa ajili ya kuihujumu timu hiyo ifungwe na Kagera Sugar.Somoe anatuhumiwa na makomandoo hao, kufanya mazungumzo na wachezaji wa Kagera Sugar, saa chache kabla ya pambano lao na Yanga, wakidai alikuwa amepewa fedha na mahasimu wa timu hiyo kuhakikisha Kagera wanashinda.
Kutokana na vitisho hivyo, tayari tukio hilo limeripotiwa katika kituo cha Polisi Kirumba jijini Mwanza na kupewa kumbukumbu MZN/RB/8712/2012.
Vitisho hivyo vilitolewa baada ya mmoja wa makomandoo hao aliyetambulika kwa jina la Saidi, kuwavaa waandishi wa habari waliofikia katika Hoteli ya Victoria Prince iliyopo eneo la Kirumba, na kutoa vitisho. Alitaka salamu hizo afikishiwe Kapinga.
Kama haitoshi, jana asubuhi kupitia simu namba 0656555599 Kapinga alipigiwa na kupewa ujumbe; “Tutakufanyia kitu mbaya kwa sababu ulikwenda Kagera kwenda kuiua Yanga,” kisha simu ilikatwa.Baada ya kuifuatilia nambari hiyo, imejulik
No comments:
Post a Comment