MKUU
wa majeshi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, amesimamishwa kazi
huku uchunguzi ukiendelea kufuatia madai kuwa aliwauzia silaha makundi
ya waasi yanaopambana na serikali ya nchi hiyo.
Ripoti
moja ya Umoja wa Mataifa, imemtuhumu, Generali Gabriel Amisi kwa
kuendesha mtandao wa kusambaza silaha kwa wawindaji haramu na makundi ya
waasi, likiwemo kundi la Mai Mai Raia Mutomboki.
Msemaji wa serikali ya nchi hiyo amesema, maafisa kadhaa wa jeshi pia wanachunguzwa.
Serikali
ya Rais Kabila imemfuta kazi mkuu huyo wa majeshi, siku chache baada ya
waasi wa M23 kuuteka mji wa Goma Mashariki mwa nchi hiyo.
Waasi
hao mpia wameutekja mji wa Sake, lakini msemaji wa serikali Lambert
Mende, amesema wanajeshi wa serikali wamefanikiwa kuumboa tena mji huo
mdogo.
Waasi
hao ambao wanaaminika kuungwa mkono na serikali za Rwanda na Uganda,
wametishia kuendeleza mapigano hayo hadi mji mkuu wa Kinshasa, ikiwa
rais Joseph Kabila hatabuli kuanzisha mazungumzo ya amani.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment