Kwa mujibu wa taarifa alizozipata Nicomedes Kajungu na kuutaarifu umma wa Wanamabadiliko Tanzania:MHASHAMU Askofu Mkuu wa Kanisa katoliki Jimbo la Shinyanga, Aloysius Balina, amefariki dunia katika hospitali ya rufaa ya Bugando alikokuwa akitibiwa.
Mhashamu Askofu Aloysius Balina alizaliwa Juni 21, 1945 katika kijiji cha Isoso Ntuzu wilayani Bariadi mkoani Shinyanga na aliwekwa wakfu na Papa Yohane Paulo II mwaka 1984 kuwa Askofu wa Geita na kusimikwa Machi 10, 1985. Septemba 23, 1997 alihamishiwa Jimbo la Shinyanga na kuwa Akofu wa tatu wa Jimbo la Shinyanga hadi alipofariki.
No comments:
Post a Comment