WASANII
wa filamu za vichekesho hapa nchini, jana walionyesha kusikitishwa kwao
na kifo cha msanii mwenzao, Sharo Milionea kilichotokea Muheza, Tanga
kwa ajali ya gari jana usiku.
Wakizungumza
na saluti5 Mwananyamala kwenye msiba wa John Maganga, wasanii Kitale,
Bingwa Rivaz, Maringo Saba, Mkono, Eric na wengine wengi, walisema
wamepoteza jembe katika fani yao.
“Wasanii
wengi wa komedi haswa sisi vijana bado ni masikini sana na
hatuthaminiwi, lakini Sharo tayari alikuwa ni balozi wetu katika njia
kutukomboa kutoka hali ya kudharauliwa hadi hadhi za juu” alisema
Maringo Saba wa kipindi cha Mizengwe cha ITV.
“Sharo
alionyesha njia, alitufungua macho kuwa komedi ukiipeleka kwenye muziki
ina lipa na sote tulikuwa nyuma yake, alikuwa anatupa changamoto na
kila mtu alitamani kuwa yeye” anasema Alex wa Machejo “Bingwa wa Rivaz”.
Erick
anaye igiza sauti ya kitoto kwenye komedi zinazorushwa Channel 10
nayependa alisema Sharo ni tochi itakayoendelea kuwamulikia njia kwa
miaka mingi ijayo”.
Kwa ujmla kila msanii alijaribu kuonyesha kuwa Sharo alikuwa mtu wa watu na jinsi ambavyo pengo lake haliwezi kuzibika.Via saluti5.com
No comments:
Post a Comment