MKALI wa muziki wa kizazi kipya, Elias Barnaba ‘Barnaba’,
anajipanga kufyatua albamu yake ya tatu itakayokuwa na nyimbo kumi,
ikibebwa na jina la wimbo ‘Nimeona’.
Barnaba alisema jana kuwa albamu hiyo ataisambaza mwanzoni mwa mwaka
ujao kwani sasa yuko katika hatua za mwisho za kuikamilisha.Alisema katika albamu hiyo kutakuwa na nyimbo nyingi ukiwemo ‘Sorry’
ambao unafanya vizuri katika vituo mbalimbali vya redio, ikiwa ni wiki
mbili tangu uanze kusikika.
“Hadi sasa hivi nina nyimbo tano ambazo ziko tayari na naendelea
kuziandaa, naomba mashabiki wangu waipokee vizuri albamu hiyo ambayo
naamini itakuwa gumzo mitaani kutokana na nyimbo zilizomo ndani yake.
Mbali ya albamu hiyo, Barnaba amekuwa akiwika na albamu zake kama
‘Kilicho Changu’ na ‘Njia Panda’ ambazo zilifanya vizuri na kumweka
kwenye nafasi nzuri kisanii.
No comments:
Post a Comment