MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Sunday Mangu ‘Linex’,
anamshukuru Mungu kibao chake cha ‘Aifola aifola’ kinafanya vizuri
kwenye tasnia ya muziki wa kizazi kipya kutokana na ujumbe ulio ndani
yake.
Linex alisema jana kuwa huo ni wimbo wenye ujumbe mzito katika jamii
na hasa kwa wanandoa, hivyo ni muhimu kwa wahusika kuusikiliza na
kuufanyia kazi ili kuwa na ndoa ya amani na upendo.
“Wakati ngoma hiyo inaingia sokoni, wengi walinishangaa kwa kuiita
jina hilo, lakini naona wananipa sapoti. Na wengi wao wananipongeza kwa
mashairi yaliyomo kwenye ngoma hiyo,” alisema Linex.
Nyota huyo anawasihi wapenzi wa muziki wa kizazi kipya kuendelea kumpa
sapoti katika kazi zake na kwamba kuna vitu vingi ambavyo ameawaandalia
wakae mkao wa kula.
Mbali ya kibao hicho, Linex amewahi kutamba na vibao kadhaa kama Moyo
wa Subira, Mama Halima na nyinginezo kali zilizomtambulisha kwenye
muziki wa bongo fleva.
No comments:
Post a Comment