Na Victor Eliud, Geita
MKUU wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Saidi Mwema, ameeleza kushtushwa na matukio sita ya mauaji ya vikongwe yaliyotokea wilayani Chato, Geita kwa imani za kishirikina kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita.
Kutokana na hali hiyo, ameziagiza kamati za Ulinzi na Usalama za wilaya na mkoa huo kushirikiana na makundi ya kijamii wakiwemo waandishi wa habari kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara hayo.
MKUU wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Saidi Mwema, ameeleza kushtushwa na matukio sita ya mauaji ya vikongwe yaliyotokea wilayani Chato, Geita kwa imani za kishirikina kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita.
Kutokana na hali hiyo, ameziagiza kamati za Ulinzi na Usalama za wilaya na mkoa huo kushirikiana na makundi ya kijamii wakiwemo waandishi wa habari kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara hayo.
IGP Mwema alitoa kauli hiyo baada ya kusomewa taarifa ya Wilaya ya
Chato na Mkuu wa wilaya hiyo, Rodrick Mpogolo, ambayo ilionyesha kuwa
kati ya matukio 55 ya uhalifu yaliyotokea katika kipindi cha Septemba na
Oktoba mwaka huu, jumla ya vikongwe sita wameuawa.
Kamati za Ulinzi na Usalama, watendaji wa serikali na waandishi wa
habari mnalo jukumu kubwa kuelimisha jamii juu ya mauaji ya vikongwe na
kwa kufanya hivyo kwa umoja wenu tatizo hili litakwisha,” alisema IGP
Mwema aliyekuwa katika ziara ya kikazi ya siku moja wilayani humo kwa
lengo la kuzindua kituo cha polisi cha wilaya na ujenzi wa nyumba tisa
za kuishi askari.
Aidha alisema Jeshi la Polisi nchini limejiwekea mikakati mbalimbali
itakayotumika kuhahakikisha usalama wa nchi ikiwa ni pamoja na kutumia
mtandao wa teknolojia ambao unawataka askari wote kuacha simu zao wazi,
ili kuwasiliana na raia pindi kunapotokea uhalifu wowote.
“Tutatumia pia alama za vidole kutambua mhalifu kwa kujua makosa yake
yote aliyotenda kipindi cha nyuma, kuwawezesha askari kubobea katika
mafunzo kupitia chuo cha polisi,” alisema Mwema.
Katika hatua nyingine, amewaonya askari wanaojihusisha na vitendo vya
kupokea rushwa kwa lengo la kupindisha tuhuma zinazowakabili watuhumiwa
na kuacha kutumia silaha kwa wananchi katika kukabiliana nao, ili
kudhibiti madhara ya matukio ya mauaji na kwamba askari atakayebainika
kujihusisha na tabia hiyo atachukulia hatua kali za kisheria.
Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, alisema matukio ya
wananchi kujichukulia sheria mikononi inatokana na askari kuzidisha
upole kwa raia hasa wakati wa kukabiliana nao.
“IGP Mwema, hatua ya wananchi kujichukulia sheria mikononi mbele ya
askari inatokana na askari kuzidi upole, waambie wawe wakali zaidi
wanapokuwa wapole nchi haitatawalika, wananchi wataendelea kuchoma moto
vituo vya polisi,’’ alisema Magufuli ambaye pia ni mbunge wa Chato.
Ujenzi wa kituo hicho uliogharimu sh milioni 50 unatokana na kituo
kilichokuwepo kuteketezwa kwa moto na wananchi Oktoba 7, 2007 kwa kile
kilichodaiwa na wananchi hao kushinikiza kumtoa mwanamke mmoja aliyekuwa
amehifadhiwa kituoni hapo baada ya kubainika kuwa alikuwa na ngozi ya
binadamu.
No comments:
Post a Comment