Afrika kusini inawania taji lake la pili
Baada ya Libya kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe,
shirikisho la soka barani Afrika liliamua mwaka jana kuwa fainali za
mwaka 2013 zifanyike nchini Afrika kusini. Timu ya nchi hiyo kama
inavyojulikana "Bafana Bafana", inaweza kutwaa taji hilo kwa mara ya
pili baada ya kuwa mabingwa mwaka 1996. Afrika kusini imo katika kundi A
pamoja na Angola, Cape Verde na Morocco.
Angola yatumai kufanya vizuri mara hii
Kwa mara ya saba Angola imefanikiwa kucheza katika fainali za kombe
la Afrika. Timu hiyo inayofahamika kama "Palancas Negras", ilifanikiwa
kwa kuiondoa Zimbabwe kwa mabao 3-1 katika mchezo wa kwanza na kuiadhibu
Zimbabwe tena kwa mabao 2-0 nyumbani mjini Luanda. Magoli yote mawili
yalifungwa na mshambuliaji Manucho (kulia).Mashabiki wa Angola wameonyesha matumaini kuwa timu yao (pichani) itafanikiwa kuvuka kikwazo cha duru ya kwanza. Wanahisi kuwa ushindi unawezekana dhidi ya wenyeji Afrika kusini, Morocco na Cape Verde. Kocha wa Angola, raia wa Uruguay, Gustavo Ferrín, kwa upande wake analiona kundi A kuwa gumu zaidi. Côte d'Ivoire haitakubali tena kuwa ya pili
Côte d'Ivoire inakwenda katika fainali hizo nchini Afrika kusini
ikiwa ni makamu bingwa. Côte d'Ivore imeishinda Senegal katika awamu ya
kufuzu katika makundi. Mjini Dakar baada ya Côte d'Ivoire kuongoza kwa
mabao 2-0, kulizuka ghasia na mchezo kuvunjika. Senegal iliondolewa.
Côte d'Ivoire inacheza katika kundi D pamoja na Tunisia, Algeria na
Togo.
Togo: Timu yenye wasiwasi
Mara sita Togo imeshiriki katika fainali za kombe la Afrika, na mwaka
2006 ilishiriki katika fainali za kombe la dunia nchini Ujerumani.
Mwaka 2010 timu hiyo ilijitoa katika fainali zilizofanyika nchini Angola
baada ya basi la timu hiyo kushambuliwa na waasi wanaotaka kujitenga
katika jimbo la Cabinda. Watu watatu walikufa. Togo imo katika kundi D
pamoja na Côte d'Ivoire, Tunisia na Algeria.
Baada ya kushiriki kwa mara ya kwanza mwaka 2012 Niger inarejea
nchini Afrika kusini kwa mara ya pili.Timu hiyo inayojulikana kama
"Menas", kwa lugha ya Kihausa, ina maana ya mnyama paa. Mlinzi Mohamed
Chocoto (pichani) anayechezea timu ya AS Marsa ya Tunisia ni mmoja kati
ya wachezaji maarufu wa timu hiyo. Niger imo katika kundi B ikiwa pamoja
na Ghana, Mali, na Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.
Morocco: Simba wa milima ya Atlas
"Simba" iliisambaratisha Msumbiji kwa mabao 4-0 mjini Marrakesh na
kufanikiwa kukata tiketi yao kwa fainali hizo za Afrika kusini. Morocco
katika mwaka 1986 ilikuwa timu ya kwanza ya kiafrika kuwa mshindi wa
kundi lake katika kombe la dunia, dhidi ya Uingereza, Poland na Ureno.
Mwaka 1976 ililitwaa kombe la Afrika. Morocco imepangwa katika kundi A
pamoja na Afrika kusini, Angola na Cape Verde.
Tunisia: Mshiriki wa kila mara
Kwa mara ya 15 Tunisia imekuwa katika fainali za kombe la Afrika.
Mwaka 2004 Tunisia ilishinda taji hilo ikiwa mwenyeji wa mashindano
hayo. Mwaka 1978 Tunisia iliandika historia kwa kuishinda Mexiko kwa
mabao 3-1 katika fainali za kombe la dunia huko Argentina. Ilikuwa
ushindi wa kwanza katika kombe la dunia kwa timu ya kiafrika. Tunisia
imo katika kundi D pamoja na Côte d'Ivoire, Algeria na Togo.
Burkina Faso inataka kuonyesha maajabu
Burkina Faso si vigogo wa soka barani Afrika. Matokeo mazuri kwa timu
hiyo yamepatikana katika fainali za 1998 iliposhika nafasi ya nne.
Tangu 1996 Burkina Faso imefanikiwa kila mara kufuzu kucheza katika
fainali. Nyota wa timu hiyo ni mshambuliaji Moumouni Dagano (pichani)
anayecheza nchini Qatar katika timu ya Al-Sailiya. Burkina Faso imo
katika kundi C pamoja na Zambia, Nigeria na Ethiopia.
Wageni wa mashindano hayo Cape Verde
Wacape Verde wanajisikia fahari na kikosi chao cha "Nyangumi wa
Buluu", ama kama wanavyofahamika nchini humo "Tubarões Azuis". Kwa mara
ya kwanza nchi hiyo inashiriki katika mashindano makubwa ya kimataifa.
Januari 19 Cape Verde itafungua dimba la fainali hizo dhidi ya wenyeji
Afrika kusini mjini Johannesburg.
Cape Verde
Cape Verde iliitoa mashindanoni vigogo wa soka barani Afrika, Simba
kutoka Cameroon kwa kuwapiga mabao 2-0 mjini Praia kutokana na uwezo wa
kocha Lúcio Antunes. Ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa marudio
haukunusuru Simba. Cape Verde hata hivyo inakabiliwa na kazi ngumu dhidi
ya Afrika kusini, Morocco na Angola katika kundi A. Kuna uwezekano
mkubwa wa kuaga mashindano katika duru ya mwanzo.
Ghana yawania taji lake la tano
Mara nne Ghana imekuwa mabingwa wa Afrika. Mara nane timu hiyo ya
Afrika magharibi imejikuta katika fainali. Mara ya mwisho ilikuwa nchini
Angola mwaka 2010. Ghana ilishindwa na Misri kwa bao 1-0. Mchezaji
maarufu katika timu hiyo alikuwa mchezaji wa kati André Ayew (kulia)
kutoka Olympique Marseille. Ghana imo katika kundi B pamoja na Mali,
Niger na Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.
Timu ya Ghana
Nigeria: Kiwango cha juu tangu miaka kadhaa
"Tai wa kijani", ni moja kati ya timu bora kabisa barani Afrika.
Mwaka 1994 Nigeria ilifikia nafasi ya tano katika orodha ya FIFA ya timu
bora duniani, ikiwa ni kiwango bora kabisa kwa timu kutoka Afrika hadi
sasa. Mwaka 1980 na 1994 Nigeria ilishinda kombe hilo la Afrika.
Ilishika nafasi ya tatu mwaka 2002, 2004, 2006 na 2010. Nigeria imo
katika kundi C pamoja na Zambia, Burkina Faso na Ethiopia.
Mali inakuja juu
Mali imetumbukia katika matatizo ya kisiasa kutokana na kujitenga kwa
upande wa kaskazini unaodhibitiwa na makundi ya Waislamu wenye imani
kali. Pamoja na hayo, Mali imefanikiwa kukata tiketi ya fainali za 2013.
Katika fainali za 2012 nchini Guinea ya Ikweta na Gabon, timu hiyo
ilifanikiwa kushika nafasi ya tatu. Mali imo katika kundi B pamoja na
Niger, Ghana na Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.
Burkina Faso inataka kuonyesha maajabu
Burkina Faso si vigogo wa soka barani Afrika. Matokeo mazuri kwa timu
hiyo yamepatikana katika fainali za 1998 iliposhika nafasi ya nne.
Tangu 1996 Burkina Faso imefanikiwa kila mara kufuzu kucheza katika
fainali. Nyota wa timu hiyo ni mshambuliaji Moumouni Dagano (pichani)
anayecheza nchini Qatar katika timu ya Al-Sailiya. Burkina Faso imo
katika kundi C pamoja na Zambia, Nigeria na Ethiopia. ![Burkina Faso inataka kuonyesha maajabu](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_sIKZxVlccd3u9oMTeI-r9CqEcyMNxN5pDFE7LAXfjMSUjuLZP5parriiDyfauCyqodycSrhS_ilTloPeZavjGq3IZ-PXoJD7yVtF3OkIvCoQ=s0-d)
Burkina FasoEthiopia inakabiliwa na changamoto kubwa
Kwa muda wa chini ya mwaka mmoja kocha Sewnet Bishaw amefanikiwa kuiwezesha Ethiopia kufuzu kucheza katika fainali za kombe la Afrika ambapo kwa muda wa miaka 31 Ethiopia ilishindwa kushiriki. Mwaka 1962 Ethiopia ilitawazwa mabingwa wa Afrika, wakati mashindano hayo yalipofanyika nchini humo. Pamoja na mabingwa watetezi Zambia, Nigeria na Burkina Faso, Ethiopia inarejea dimbani katika kundi C.
No comments:
Post a Comment