MKUTANO wa mwaka wa wanachama wa Yanga unatarajiwa kufanyika Jumamosi hii katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaa.
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako alisema mkutano huo wa wanachama ni kwa ajili ya kuzungumzia mambo ya klabu yao pamoja na Ligi Kuu Tanzania Bara.
Pia Mwalusako alisema klabu yao imeingia mkataba wa mwaka mmoja na kampuni ya Apecha Media Promotion kwa ajili ya kutengeneza kalenda ya klabu hiyo.
Alisema kuwa mkataba huo ni moja ya hatua na mwanzo mzuri hivyo amezitaka kampuni nyingine kujitokeza kutengeneza vitu vingine kwa ajili ya maendeleo ya klabu yao.

No comments:
Post a Comment