WANATAALUMA wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Udasa), wameandaa
kongamano litakalofanyika Desemba 9, mwaka huu, ambalo litazungumzia
uhuru na mustakabali wa taifa kwa miaka 50 ijayo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam,
Mwenyekiti wa Udasa, Dk. Francis Michael, alisema kuwa kongamano hilo
litahusisha pia mada ndogo zinazohusu amani na utulivu wa taifa, elimu
na maendeleo ya taifa pamoja na rasilimali na maendeleo kiuchumi.
Alisema dhamira ya kuandaa kongamano hilo ni kuchochea mjadala endelevu kuhusu mustakabali wa taifa letu.
“Kwa sasa tumechagua maeneo hayo machache kwani yana athari;
mtambuka…amani ya kweli na utulivu nchini vikiendelea kuwepo, wananchi
watafanya shughuli za kiuchumi kwa mafanikio,” alisema.
Aliwataja wazungumzaji wakuu katika kongamano hilo kuwa ni Profesa
Gaudence Mpangala, mwandishi wa habari Maggid Mjengwa, Dk. Martha Qorro,
Dk. Kitila Mkumbo na Dk. Haji Semboja
No comments:
Post a Comment