Na Berensi Alikadi-Tanzania Daima.
MWANAHARAKATI wa Haki za Binadamu Mkoa wa Mara, Eustace Nyaruganda (45) amekutwa amekufa katika nyumba ya kulala wageni (gesti).
MWANAHARAKATI wa Haki za Binadamu Mkoa wa Mara, Eustace Nyaruganda (45) amekutwa amekufa katika nyumba ya kulala wageni (gesti).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Ofisa
Shughuli wa Shirika la ABC Foundation, Andreas Migiro, alisema alipokea
taarifa za msiba wa mkurugenzi wake jana asubuhi baada ya kupigiwa simu
na meneja wa ofisi yao.
Migiro alisema alipewa taarifa kuwa mkurugenzi wao alikutwa jana asubuhi
akiwa amekufa katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la
Savana iliyoko Mtaa wa Benki mjini Bunda.
“Kwa kweli nimeshutushwa na kifo cha huyu mkurugenzi wetu maana
ikumbukwe kuwa mwaka jana alipotea katika mazingira ya kutatanisha na
baadaye alipatikana, na juzi tena alipotea na leo nimepata taarifa za
kifo chake,” alisema Migiro.
Akizungumzia kifo hicho, Mratibu wa mtandao wa kutetea haki za binadamu
nchini, Onesmo ole Ngulumwa, alisema wamepokea kwa masikitiko makubwa
taarifa za kifo hicho na kwamba ni pigo kwa watetezi wa haki za
binadamu.
Hata hivyo, baadhi ya wanaharakati wanaohudhuri mafunzo hayo wameonyesha
kusikitishwa na mazingira ya kifo hicho ambapo wamesema kuwa hivi sasa
maisha ya wanaharakati yako hatarini, hivyo ni lazima waishi kwa
tahadhari.
No comments:
Post a Comment