EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, January 18, 2013

MADARAKA YA RAIS YAWAGAWA VIGOGO NCHINI.

KWA UFUPI
“Napendekeza kwamba Katiba Mpya iangalie upya madaraka ya Rais katika uteuzi wa viongozi wa umma, lakini masuala mengine yanayomhusu Rais katika utendaji kazi wake.Waziri Mkuu Mstaafu John Malecela akizungumza na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliokutana nao jana, ili kutoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya. Kulia ni Makamu Mwenyekiti Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na Mjumbe wa Tume Prof. Mwesiga Baregu.Picha ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba .
VIONGOZI waandamizi wastaafu wa Serikali, John Malecela, Frederick Sumaye na Barnabas Samatta wametofautiana kuhusu madaraka ya Rais yanavyostahili kuwa katika Katiba Mpya.

Katika maoni waliyotoa jana mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mawaziri Wakuu wastaafu, Malecela na Sumaye walitoa misimamo hiyo inayopingana kwa nyakati tofauti jana.

Wakati Malecela akitaka Katiba Mpya isiguse madaraka ya Rais kwa namna yoyote ile, Sumaye amependekeza viongozi anaowateua mkuu huyo wa nchi, wathibitishwe na vyombo vingine.

Msimamo wa Sumaye haukutofautiana sana na ule wa Jaji Mkuu mstaafu, Samatta ambaye amependekeza madaraka ya Rais yaangaliwe upya katika kipengele cha uteuzi wa viongozi wa umma na utaratibu wa kuwapata majaji.

“Napendekeza kwamba Katiba Mpya iangalie upya madaraka ya Rais katika uteuzi wa viongozi wa umma, lakini masuala mengine yanayomhusu Rais katika utendaji kazi wake yabaki kama yalivyo kuwa sasa,” alisema Jaji Samatta.

Akizungumza muda mfupi baada ya kuwasilisha maoni yake kwa Tume ya Katiba, Jaji Samatta alisema anataka Katiba Mpya itazame upya madaraka ya Rais katika uteuzi wa viongozi wa umma ili kuwe na mgawanyo mzuri katika nafasi hizo.

Jaji Samatta alipendekeza pia utaratibu wa kuwapata majaji utazamwe upya na Katiba Mpya iseme kwamba mawaziri hawapaswi kuwa wabunge.

“Kama tunataka maendeleo katika Mhimili wa Mahakama ni vyema Katiba Mpya ikaweka utaratibu mpya wa kuwapata majaji.

Napendekeza Katiba Mpya iweke utaratibu wa kuwapata majaji ili kuhakikisha tunaboresha upande wa Mahakama zetu.”

“Utaratibu huo utasaidia kwa kiwango kikubwa kuboresha Mahakama zetu jambo ambalo litakuwa jema kwani zitafanya kazi kwa kiwango cha juu.”

Viongozi wabanwe.
Jaji Samatta alisema Katiba Mpya ni vyema ikaunda chombo maalumu kitakachokuwa kinawabana viongozi wa umma ambao hawafanyi kazi zao ipasavyo.

Alisema chombo hicho kama kitatambulika kikatiba, kitasaidia kuondoa matatizo mbalimbali ya utendaji wa viongozi wa umma katika masuala ya maendeleo.

“Kumekuwa na malalamiko mengi ambayo yanawahusisha viongozi wa umma hasa kwa kutowajibika kwa wananchi, sasa ni vyema Katiba Mpya ikaunda chombo kitakachokuwa kinawabana viongozi wasiofanya kazi zao ipasavyo,” alisema.

Pia Jaji Samatta alipendekeza Katiba Mpya ikataze mawaziri kuwa wabunge ili kila mmoja afanye kazi zake ipasavyo.

Sumaye.
Sumaye alitaka viongozi wanaoteuliwa na Rais wathibitishwe na vyombo vingine akitolea mfano uteuzi wa majaji na watumishi mbalimbali wa juu katika Serikali... “Rais anaweza kuwateua, lakini Bunge linaweza kushiriki kuwapitisha watu hao.”

Pia alipendekeza nafasi za wakuu wa wilaya ziendelee kuwepo lakini zisiwe za kisiasa.

Malecela.
Akizungumzia madaraka ya Rais, Malecela alisema anawashangaa watu wanaotaka Rais apunguziwe madaraka na akapendekeza Katiba Mpya kumpa nguvu ili aendelee na madaraka aliyonayo sasa.

Alisema haoni kama kuna haja ya kumpunguzia Rais madaraka kwani tayari kuna mihimili mingine ya dola.

“Nawashangaa watu wanaotaka Rais apunguziwe madaraka. Mimi naona hakuna haja ya kufanya hivyo kwani tayari kuna mihimili mingine ya dola ambayo inafanya kazi zake kwa kujitegemea,” alisema Malecela na kuongeza:

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate