WAZEE wa Kibega, Mashujaa Band wamepania kuja kivingine kwa mwaka huu wa 2013 ili kupiga hatua moja mbele kutoka pale walipo.
Meneja wa bendi hiyo, Martin Sospeter, ameiambia Saluti5 kuwa kwa malengo waliyojiwekea, mwaka 2013 utashuhudia mageuzi makubwa kutoka kwao.
Kwasasa
wanamuziki pamoja na safu ya utawala tumeshashikana na kila mmoja
ameelewa wajibu wake, mwaka uliopita ulikuwa wa kuwekana sawa na kuzoea
hali ya hewa, sasa tunaanza rasmi kazi ya kuligeuza soko la muziki chini
juu” alitamba Martin.
Aidha
Martin amesema wamegundua mapungufu machache katika baadhi ya idara
kwenye bendi yao na muda si mrefu watafanya usajili mwingine
utakaotinginsha nchi.
“Tutafanya usajili wa kishindo, aidha kutoka nje ya nchi au ndani ya nchi” alisema Martin bila kufafanua.
Kwa
kawaida Mashujaa Band wanapatikana Business Park Kijitonyama kila siku
za Ijumaa na Jumapili, wakati kila Ahamisi wanakuwa ndani ya ukumbi wa
Sun Cirro Sinza.
Via saluti5
No comments:
Post a Comment