EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, January 9, 2013

Mtuhumiwa kesi ya Dk. Ulimboka aishika pabaya serikali... Aishi juu ya paa la Gereza Keko, agoma kula.

RAIA wa Kenya, Joshua Mulundi, anayekabiliwa na kesi ya kumteka na kutaka kumsababishia kifo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Chama cha Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka, ameanza mgomo wa kula na ameamua kuishi juu ya paa la Gereza la Keko akitishia kutaka kujiua.

Mtuhumiwa huyo ambaye Jumapili iliyopita kupitia gazeti la Tanzania Daima Jumapili alitoboa siri ya jinsi alivyokamatwa na kutoa kauli nzito kulalamikia mwenendo wa kesi yake, amefikia hatua hiyo kwa lengo la kuishinikiza serikali imlete mbele yake Dk. Ulimboka ili afanyiwe gwaride la utambulisho kubaini kama alihusika katika tukio la kumteka.

Akizungumza na gazeti hili juzi kutoka ndani ya Gereza la Keko, Joshua alisema kuanzia jana alitarajia kuanza mgomo wa kutokula na atakuwa akiishi juu ya paa la gereza hilo kwa lengo la kuishinikiza serikali ikamilishe uchunguzi wa kesi yake.
Habari kutoka ndani ya Gereza la Keko ambako mtuhumiwa huyo amehifadhiwa, zilisema kuwa raia huyo wa Kenya ameanza mgomo jana.

Imeelezwa kuwa amechukua uamuzi huo mgumu baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa kesi ambayo tangu Julai 3, mwaka jana bado iko kwenye hatua ya upelelezi na hajui utakamilika lini.
Askari mmoja wa Jeshi la Magereza kutoka ndani ya gereza hilo alikiri kuwa mtuhumiwa huyo amegoma na usiku wa kuamkia jana alishinda juu ya paa la gereza huku mvua ikimnyeshea.

“Ni kweli huyo bwana amegoma, uongozi wa gereza umefanya juhudi za kuzungumza naye na kilio chake anasema anataka upelelezi wa kesi yake ukamilike haraka ili atendewe haki, lakini kubwa kuliko yote, ameitaka serikali imlete Dk. Ulimboka mahakamani ili aweze kumtambua,” alisema askari huyo.

Habari zaidi zinasema kuwa ndugu wa mtuhumiwa huyo ambaye hana wakili mahakamani, wamewasili kutoka nchini Kenya kwa ajili ya kutoa msaada wa kisheria.
Kwa mujibu wa ndugu hao, hadi sasa hawaoni maendeleo ya kesi hiyo kwani kila ikifika mahakamani upande wa mashitaka hutoa hoja ya kutaka iahirishwe kwa madai kuwa upelelezi haujakamilika.

Juzi mtuhumiwa wa kesi hiyo inayovuta hisia za wengi nchini aliliambia gazeti hili kuwa amepata kutoa malalamiko kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), akiiomba serikali imlete mbele yake, Dk. Ulimboka ili amtambue na kuhakikisha upelelezi wa kesi hiyo unafikia tamati.
Mbali ya maombi hayo, mtuhumiwa huyo pia alisema aliwaomba viongozi hao wamsaidie kupata dhamana kwani kesi inayomkabili inaruhusu dhamana na hana wakili wa kumtetea.

Dk. Ulimboka ajipa muda
Wakati Joshua akitaka afanyiwe gwaride la utambulisho, kwa upande wake Dk. Ulimboka alisema kwa sasa hana cha kusema, lakini muda ukifika atasema ukweli wote.
Alisema hajawahi kuitwa na kukutanishwa na mtuhumiwa wa kesi hiyo wala hajaombwa kuwa mmoja wa mashahidi, ingawa anajua atatakiwa kwenye ushahidi.
“Mimi sina la kusema kwa sasa, naviachia vyombo husika kufanya kazi yao, lakini muda ukifika naweza kusema lolote, ila kwa sasa tuviachie vyombo vya dola,” alisema Dk. Ulimboka.

Magereza wang’aka
Kwa upande wake, Jeshi la Magereza nchini limegoma kuzungumzia mgomo wa mahabusu huyo na hatua anazochukua gerezani kushinikiza kesi yake iendeshwe haraka.
Msemaji wa jeshi hilo, Danstan Lissu, alipoulizwa na gazeti hili alikuwa mbogo na kuhoji gazeti hili limepataje taarifa za mgomo wa mahabusu huyo.

“Taarifa hizi umepata wapi? Nani amekuambia? Siwezi kulizungumzia suala hilo kwa vile sijaruhusiwa, mtafute Kamishna Mkuu wa Magereza akupe taarifa hiyo,” alisema Lissu.
Hata hivyo Tanzania Daima Jumatano ilipomtafuta Kamishna Mkuu wa Magereza, John Minja, kupata taarifa juu ya mahabusu huyo hakuweza kupatikana na simu yake ya mkononi ilikuwa ikiita bila majibu.

Dk. Ulimboka ambaye alikuwa kinara wa mgomo wa madaktari uliotikisa nchini kwa wakati tofauti mwaka jana; alitekwa, kuteswa, kupigwa hadi kung’olewa meno na kucha na kisha kutupwa katika msitu wa Mabwepande, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Baada ya tukio hilo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alitangaza kuunda tume ya wataalamu kutoka ndani ya jeshi hilo, iliyoongozwa na ACP Ahmed Msangi.

Hatua hiyo ilikuja baada ya Dk. Ulimboka mwenyewe kuwataja baadhi ya watu aliodai kuwa ndio walihusika kumteka na kumtesa, lakini hadi sasa Mulundi ndiye mtuhumiwa pekee aliyekamatwa.

Hata hivyo tume hiyo haijawahi kutoa ripoti yake kama Kova alivyoahidi pamoja na kwamba hata majeruhi mwenyewe, Dk. Ulimboka hajawahi kuhojiwa, huku vigogo wa jeshi hilo wakitupiana mpira kuhusiana na sakata hilo.
Hivi karibuni jeshi hilo kupitia kwa msemaji wake, Advera Senso, limekanusha kuwapo kwa tume hiyo, likisema walioteuliwa ni polisi ambao watafanya kazi za kiuchunguzi kwa taratibu za polisi.

Kauli ya Senso ilipingana na ile ya Kova, ambaye hivi karibuni alikiri kuwapo kwa tume hiyo, lakini akasema hawezi kulizungumzia suala hilo kwa vile taarifa zake alishazipeleka kwa wakubwa wake makao makuu baada ya kukamilisha wajibu wake.
Wakati vigogo hao wakisigana katika kulifafanua sakata hilo, Dk. Ulimboka mara kadhaa amekuwa akieleza kuwa yupo tayari kutoa maelezo yake kama kutakuwa na tume huru ambayo si hiyo iliyoundwa na polisi.

Katika tamko lake mwishoni mwa mwaka jana lililosomwa kwa niaba yake na wakili wa kujitegemea, Nanyoro Kicheere, akimwakilisha mwanasheria wake, Dk. Ulimboka alisema wapo watu ambao hawatapenda kusikia siri iliyojificha katika tukio zima la kutekwa kwake na kwamba hana jinsi zaidi ya kueleza ukweli wakati ukifika.
Alisema kuwa tukio la kutekwa na hatimaye kutupwa katika msitu wa Mabwepande, lilitokea wakati akiwa katika kikao na ofisa aliyetambulishwa kwake kuwa ni Ofisa wa Ikulu, Ramadhani Abeid Ighondu, ambaye hadi leo Ikulu haijatoa ufafanuzi kama inamtambua au la.               CHANZO CHA HII HABARI NI TANZANIA DAIMA

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate