MWALIMU Mkuu wa Shule ya Sekondari Ilkiding’a, iliyopo wilayani
Arumeru, amewakataa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha
kwanza shuleni hapo wanaotoka katika shule za msingi za Kata ya
Ilkiding’a kwa madai kuwa ni watoro na hawapendi kusoma.
Akizungumza katika kikao cha wazazi kilichofanyika shuleni hapo juzi,
Mkuu huyo, Omary Nyangu, alisema hataki kuwapokea wanafunzi wanaotoka
katika shule za msingi Kioga, Olturoto na Kiding’a, mara nyingi
wanafunzi hasa wa kike wamekuwa wakiacha shule bila sababu na kufanya
maendeleo ya shule kuzorota kutokana na takwimu kuyumba kila mwaka.
“Tatizo hili linachangiwa na wazazi ambao wamekosa maamuzi kwa watoto
wao, hivyo kuwaacha wafanye lolote watakalo bila kujua kuwa wanaharibu
malengo ya maisha yao ya baadaye,” alisema.
Mmoja wa wazazi waliohudhuria kikao hicho, Francis Elias, alisema
uamuzi alioufanya mwalimu huyo ni wa busara, kwani wanafunzi wengi
wanaotoka kata hiyo wamekuwa wakimaliza kidato cha nne na kupata sifuri,
jambo linalowakatisha tamaa wazazi.
Aliwataka wazazi kuwaelimisha watoto wao juu ya changamoto za maisha zitakazowakabili wasipokuwa na elimu.
No comments:
Post a Comment