MSANII
maarufu wa filamu na muziki hapa nchini, Baby Madaha, amesema kulingana
na nafasi yake ya kiusanii hawezi kuvaa nguo za zinazoficha sana maungo
yake.Baby Madaha amesma katika hali halisi anatakiwa kuwa tofauti na mtu wa kawaida, hivyo si rahisi kuvaa kama yupo nyumbani.
Hata hivyo Baby Madaha alifafanua kuwa anavaa nguo hizo pale anapokuwa kazini tu.
“Ni kweli navaa nguo za kujiachia, mimi ni star, lazima
niwe tofauti na mtu mwingine hatuwezi kuwa sawa na watu wasio wasanii
japo kuna watu ambao inawakera, lakini ni wazi kuwa mavazi hayo nayavaa
ninapokuwa jukwaani au nikirekodi filamu kulingana na uhusika, si
kinyume na hapo”, alisema Baby Madaha.
No comments:
Post a Comment