KAMA kuna watu wanaotakiwa kujua thamani yao na kuitumia kwa faida
basi ni wasanii wa filamu, lakini hali haipo hivyo mwaka 2012 na 2013
umekuwa ni mwaka wa matukio hususan misiba japo kulikuwa na furaha pia,
misiba ndio iliyotufanya tujue kama wasanii ni matajiri wasio na kitu
mkononi.
Msiba wa marehemu Kanumba ndio uliotufungua na kuamini thamani ya
wasanii ni kubwa lakini haikuwa rahisi kuwezesha mazishi hadi pale
ilipoundwa kamati kwa ajili ya kuchangishana pesa za rambirambi kutoka
kwa wadau mbalimbali na si wasanii wenye, vyombo vya habari vilishika
nafasi kwa kuhakikisha michango inapatikana na mazishi yakafanyika.
Jambo ambalo ni agharabu kutokea kwa mazishi yoyote katika misiba lilitokea kila kiongozi awe wa siasa Serikali alihakikisha anafika Sinza Vatican kwa ajili ya kuhudhuria msiba huo bila kadi ya mwaliko wala nini, kamati zilikusanya mamilioni ya fedha na mazishi yakafanyika lakini siku ya siku shutuma zikaja kama kuna watu walijinufaisha na mikwanja ya marehemu.
.
Hali ya kukabana kwa ajili ya wasanii wazikwe imeendelea japo kwa marehemu Sharomilionea hakuwa hivyo sijui ilikuwaja lakini hivi karibuni baada ya rafiki kipenzi cha wapenda filamu Sajuki kufariki bakuli liliendelea hadi kuna wakati watu waliokuja kuhani msiba walikuwa na hofu kama wangebanwa kutoa michango ili kupata zaidi ya milioni nane.
Swali ambalo wengi wanajiuliza pamoja na thamani ya wasanii hawa kwani haiendani na maisha yao halisi? Inasemekana kuwa wasanii hawa hawalipwi malipo stahili lakini jambo baya kuliko yote ni pale chama cha hakimiliki nja hakishiriki kugeuka kuwa wakala wa maharamia kwa kuwakandamiza wasanii kwa kuuza haki zao na kubaki kuwa watu wa mizinga.
Ni maneno yanayouma lakini ukweli ni kwamba tatizo nambari moja wasanii wenyewe hawajijui nini wanahitaji wapi na kwa wakati gani? Wasanii badala ya kuungana na kutafuta maslahi ya pamoja badala yake imekuwa ni vita ya kimaslahi wanapokutana kwa wasambazaji kila mtu akitaka kuwa ni bora kuliko mwingine jambo linalowapa nafasi wasambazaji kuendelea kuwanyonya.
Jamii inaamini kuwa wasanii ni watu wenye nafasi katika jamii lakini pengine ukweli haupo hivyo kulingana na maisha yao kuwa tegemezi kwa kila kitu, hivi karibuni mtayarishaji na mwigizaji mkongwe katika tasnia ya filamu alisema kuwa wasanii hata magari unayoyaona ukopeshwa na wasambazaji hali inayowafanya kuwa Matonya.
.
Serikali kupitia mamlaka ya mapato imesema inarasimisha filamu na muziki na tayari tunaona matangazo katika vyombo vya habari ikiwa kama sekta rasmi, lakini wasanii wanalalamika kuwa hoja kwao si kurasimisha bali wanataka haki zao zilindwe kwa sababu hawana imani na taasisi kama Cosota baada ya kuwa ajenti wa wale wanaowadhulumu haki zao, kwa kifupi ni tatizo ni mikataba na si kingine.
Sheria inasema kuwa haki miliki ya mtunzi hainunuliki hata baada ya kifo cha mtunzi, ambapo uweza kudumu kwa miaka 50 kwa nchi zilizoendelea kama Marekani ni miaka 75 kwa mantiki hiyo ina maana hawa watendaji wa Cosota hawalitambui hilo au ndio Fedha inaongea na kudhulumu haki ya wasanii na kuwa maskini pamoja nakuwa na umahiri na umaarufu usio na malipo!
No comments:
Post a Comment