THEO Walcott leo hii amesaini mkataba mpya wa miaka mitatu na nusu kuendelea kuitumikia Arsenal, mkataba wa pauni 100,000 kwa wiki.
Walcott amesema: “Nina furaha kusaini mkataba mpya Arsenal.
“Nawashukuru wote walioniunga mkono, hususan kocha, kila moja ikiwa ni pamoja na mashabiki ambao ni watu muhimu sana.
“Tangu mwanzo niliweka wazi kuwa nataka kubaki Arsenal, nina furaha kuingia mkataba mpya ambao kila mmoja ameridhika nao.
Kocha wa Aresenal, Arsene Wenger amesema: “Tunafuraha kwamba Walcott amesaini mkataba mpya.
“Alikuja hapa akiwa na miaka 16 na kutoka hapo ameimarika na kuwa mchezaji muhimu kwa Arsenal na England”
No comments:
Post a Comment