EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, January 19, 2013

Tume ya Uchaguzi yamkimbia rais

JOTO la kupunguziwa madaraka ya uteuzi kwa rais, limezidi kupanda ambapo sasa Tume ya Uchaguzi (NEC) nayo imependekeza iondolewe chini ya rais, badala yake iwe chini ya Bunge.
Tume hiyo, imesema imefikia uamuzi huo baada ya kutafakari madai ya wadau wengi ambao wamekuwa wakishutumu utendaji wake, kwamba umelenga kukipendelea Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika maamuzi yake.

Imetaka wajumbe wake wasiteuliwe na rais kama ilivyo sasa, badala yake majina yao yapendekezwe na jopo maalumu, kisha yathibitishwe na Bunge kabla ya kupelekwa kwa rais.
Kutokana na mapendekezo hayo, sasa kazi ya rais itakuwa kuteua majina ya wajumbe wa tume hiyo. Kadhalika, tume inataka rais asiwe na mamlaka ya kuwafukuza kazi wajumbe wake, bali jukumu hilo libaki mikononi mwa jopo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Tume hiyo, 

Jaji mstaafu Damian Lubuva, alisema pia wanataka wajumbe wa tume waapishwe na jaji mkuu ili kuondoa wasiwasi wa kuwa watii kwa rais ambaye pia anakuwa mwenyekiti wa chama kinachotawala.
Katika maoni yao kwa ajili ya katiba mpya, Jaji Lubuva alisema wanataka pia wajumbe wa tume wasiteuliwe kwa kuzingatia kiwango cha elimu, bali wazingatie sifa nyingine zikiwemo za uadilifu, heshima, uwajibikaji na namna anavyokubalika katika jamii ya Watanzania.

Kufukuzwa kwa kiongozi
Katika mapendekezo yake, Tume ya Uchaguzi pia imetaka kufanyika kwa mabadiliko yatakayowawezesha viongozi wa kisiasa wanaohama, ama kufukuzwa na vyama vyao kubaki katika madaraka hadi mwisho wa muda wao wa uongozi.
Jaji Lubuva alisema iwapo mbunge au diwani atafukuzwa au kuhamia chama kingine, basi ahame na kiti chake cha uwakilishi ili kuzuia matumizi makubwa ya gharama za kufanya uchaguzi mdogo.

Kwa mujibu wa utaratibu wa sasa, kiongozi wa kuchaguliwa anapofukuzwa ama kuhama chama chake, hulazimika kuachia ngazi, hivyo kuwepo kwa uchaguzi mdogo kujaza nafasi iliyoachwa wazi.
Katika mapendekezo mengine, tume inataka kuwepo na utaratibu wa wapiga kura kuwaondoa madarakani wabunge na madiwani ambao hawatawajibika katika nafasi zao, badala ya mfumo wa sasa unaoruhu kuondolewa kwa viongozi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji pekee.

Mahakama ya Uchaguzi
Mapendekezo mengine ya tume hiyo ni kuwepo kwa Mahakama ya Uchaguzi itakayowezesha wadau na wananchi wasiokubaliana na uamuzi wa tume kukata rufaa kabla ya kuwasilishwa kwa kesi za uchaguzi mahakamani.
Alisema kuwa mahakama hiyo itafanya kazi pale itakapohitajika, na muda wa kutekeleza majukumu yake uwe wa haraka kutokana na kazi za uchaguzi zilivyo.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate