MSHINDI wa Epiq Bongo Star Search (EBSS -2012), Walter Chilambo,
anajipanga kuachia ngoma yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la
‘Siachi’.
Walter Chilambo
Akizungumza na mdau wetu kupitia facebook jana, Walter
alisema yupo katika hatua za mwisho za uandaaji wa kibao hicho, ambacho
kinaelezea mkasa wa mapenzi.
Alisema ndani ya wimbo huo amezungumzia mapenzi, ambako alikuwa
anamkataa mpenzi wake na mwisho wa siku, akaja kugundua kwamba ni wa
muhimu katika maisha yake na ndiyo maana akauita wimbo huo ‘Siachi’.
“Naomba mashabiki wangu na wale wote ambao walinipigia kura, wakae
mkao wa kula kwa ajili ya kukipokea kibao hiki, ambacho naamini
kimefuata maadili ya nchi tangu,” alisema.
Walter alisema kwa sasa anajipanga kutengeneza video ya kazi hiyo
ambayo anaamini itakuwa gumzo mtaani kutokana na maudhui iliyobeba.
No comments:
Post a Comment