Timu
ya Young Africans iliyokuwa imeweka kambi ya mafunzo kwa muda wa wiki
mbili inatarajiwa kuondoka majra ya mchana mjini Antalya - Uturuki
kupitia Istambul ambapo inatarajiwa kuwasili uwanja wa ndege wa
kimataifa JNIA Dar es salaam majira ya saa 10 kasorobo kwa saa za Afrika
Mashariki.
Young Africans ambao ni Mabingwa mara 23 wa Ligi Kuu ya
Tanzania bara na Bingwa mara tano (5) wa kombe Vilabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati iliweka kambi ya mafunzo katika mji wa Antalya kwa
muda wa takribani siku 14 ambapo ilikuwa ikifanya mazoezi na kupata
fursa ya kucheza michezo mitau (3) ya kirafiki.
Katika
kambi yake ya wiki mbili Young Africans iliapata fursa ya kucheza
michezo mitatu ya kirafiki na timu za Arminia Bielefeld ya ligi daraja
la tatu Ujerumani, Dinzlispor FC ilyopo ligi daraja la kwanza nchini
Uturuki na Emmen FC iliyopo ligi daraja la kwanza nchini Uholanzai.
Akiongelea
michezo ya kirafiki mitatu waliocheza na timu za Armini Bielefeld,
Deinizlispor na Emmen Fc kocha mkuu wa Yanga Ernest Brandts amesema
michezo ilikuwa ni mizuri na wamepata nafasi ya kuona mapungufu machache
yaliyojitokeza na anaamini watayafanyia kazi na kuendelea kufanya
vizuri.
Tumecheza michezo mitatu, wa kwanza
tulitoka sare na Amrinia Bielefeleld, mchezo ulikua mzuri na timu yangu
ilicheza vizuri kwa dakika 90 zote za mchezo licha ya Arminia
kusawaisha bao dakika za lala salama huku mwamuzi aklishindwa kutoa
maamuzi sawa na mshika kibendera wake, ambapo mfungaji alikua maeotea.
Mchezo
wa pili dhidi ya Denizlispor nao pia timu ilicheza vizuri na kuweza
kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini umakini wa washambuliaji
ulitukosesha ushindi kwani Tegete alitumia nafasi aliyoipta kufunga bao
la mapema kabla ya Waturuki hawajasawazisha kwa bao la utata kisha
kupewa penati ya utata pia.
Mchezo wa mwisho dhidi
ya Emmen FC ulikuwa mzuri pia na kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza
tuliutawala mchezo na kupata nafasi kadhaa za kufunga mabao lakini
kutokua makini wa washambuliaji wetu pia kulichangia sisi kukosa
ushindi, kabla ya kipindi cha pili Emmen FC kucharuka na kupata mabo
mawili ya haraka haraka kutokana na uzembe wa walinzi na mlinda mlango
Yusuph abDUL
Tunaushukuru uongozi kwa kukubali
kutupa nafasi ya kuweka kambi Uturuki, tumkeaa pamoja kwa mda mrefu huku
tukitoka mafunzo kwa vitendo, vifaa na mahitaji yote vikiwepo ,kukiwa
na hali ya utulivu, kifupi tumejifunza mambomengi sana ya msingi ambayo
yatatusaidia kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya
Vodacom na mashindano ya kimataifa yatakayotukabili alisema 'Brandts'
Timu
itaondoka Antalya majira ya saa 9:30 mchana na kufika katika mji wa
Instabul majira ya saa 10:50 jioni , kisha baadae majira ya saa 1 na
robo usiku itaanza safari ya kuelekea Dar es es salaam ambapo
inatazamiwa kufika uwanja wa ndege wa kimataifa JNIA jumatatu majira ya
saa 10 kasoro alfajiri.
Msafara utakua na jumla ya watu 33, wachezaji 27, na viongozi 6
No comments:
Post a Comment