EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, February 20, 2013

Kashfa kidato cha 4: Watahiniwa wamchora Messi, wawapiga wabunge vijembe

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi inaweza kukumbwa na kashfa kubwa kutokana na matokeo mabaya ya kidato cha nne ya 2012 yaliyotangazwa juzi na Waziri wake, Dk Shukuru Kawambwa.
 
Kashfa hiyo inatokana na aina ya majibu yaliyoandikwa na baadhi ya watahiniwa katika mitihani hiyo, huku wengine wakikusanya vitabu vya majibu bila kujibu chochote, hali inayohusishwa na uhaba mkubwa wa walimu katika baadhi ya shule za sekondari nchini.
 

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk Joyce Ndalichako alisema wasahihishaji walikutana na mambo ya ajabu yakiwamo matusi, michoro ya vitu visivyoeleweka, mashairi na nyimbo za muziki wa kizazi kipya (bongo fleva).

“Mwaka jana tulikutana na ‘single’ yaani waliandika mashairi kwa uchache, lakini mwaka huu tumepata albamu nzima… ni vituko vitupu, wengine wanaandika mapenzi, mwanafunzi anatumia ukurasa mzima kumlalamikia mpenzi wake. Miongoni mwa yaliyoandikwa ni mpenzi, umeniacha, natamani kunywa sumu, usiku silali nakuwaza wewe…” alisema Dk Ndalichako.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili ofisini kwake Dar es Salaam jana, Dk Ndalichako alisema wanafunzi wengine waliandika malalamiko dhidi ya wabunge na uendeshaji wa Bunge.

“Unakuta mwanafunzi anaeleza anavyolishangaa Bunge… mtu anaandika… nawashangaa wabunge, wamekaa kama wapo kijiweni, wabunge wamekosa ustaarabu, badala kujadili kero za wananchi waliowachagua, wanapokea timu zilizoshinda makombe… timu ikishinda Kombe la Kagame inapokelewa bungeni. Bunge limekuwa kama kijiwe, bungeni siyo ukumbi wa starehe kama mnataka kupokea timu hizo nendeni katika ofisi zao au viwanjani…” alisema.

Alisema wanafunzi walioandika vitu visivyoeleweka walikuwa ni wengi na walichangia kwa kiasi kikubwa matokeo kuwa mabaya.

Dk Ndalichako alionyesha baadhi ya michoro hiyo ambayo inaonyesha vikaragosi ambavyo wanafunzi hao waliviita Messi (Lionel, mchezaji wa Barcelona) na zombi (ni picha za kutisha) ambazo huonyeshwa kwenye televisheni.

Sababu za kufeli
Dk Ndalichako alisema hawezi kuwa na jibu la moja kwa moja juu ya kwa nini matokeo ya mwaka huu yamekuwa mabaya, lakini akadokeza kuwa huenda yametokana na wanafunzi wengi kukosa maarifa.

Anasema mbali na waliojaza matusi na michoro, wanafunzi wengine waliofanya vibaya ni wale ambao hawakujaza chochote kwenye karatasi zao za majibu.

“Kuna baadhi ya shule unakuta darasa zima watoto hawajajibu somo fulani kwa mfano Biolojia, wanaingia tu na kuandika namba. Tuliamua kuwapigia simu walimu wao, majibu waliyokuwa wakitupa ni kuwa hawajawahi kuwa na walimu wa somo husika kwa hiyo watoto hawakuwa na cha kujaza.”

Dk Ndalichako alisema kwa ku mbukumbu zake, hakuna matokeo mabaya kama ilivyo kwa mwaka huu yaliyowahi kutokea.

“Tukiangalia tu kuanzia 2000, hakujawahi kutokea matokeo mabaya kama haya, kwa kweli hali haipendezi. Hata kabla ya kuyatangaza nilikuwa nayaangalia mara tatu tatu, sikuyapenda na inasikitisha kwa kweli,” alisema Dk Ndalichako.

Udanganyifu
Dk Ndalichako alisema hakukuwa na uvujaji wa mitihani wala udanganyifu wa ndani kwani vitendo hivyo vilidhibitiwa.
Alisema baadhi ya wanafunzi wamefutiwa mitihani yao kutokana na majibu yao kukutwa na mfanano usiokuwa wa kawaida na kutoa mfano wa wanafunzi tisa katika shule ambayo hakuitaja kwamba majibu yao yalifanana katika somo la Kiswahili.


Alisema katika somo hilo, kulikuwa na swali lililotaka wanafunzi waandike shairi la kuonyesha umuhimu wa mwalimu na kwamba wanafunzi hao waliandika shairi moja la majigambo lililofanana kwa kila kitu.

“Ni vigumu wanafunzi wote tisa kuwaza na kuandika kitu kimoja, shairi hilo lilifanana kila kitu na kwenye kiitikio wote walikosea kwa kuandika neno ‘hacheni’ niitwe mwalimu badala ya ‘acheni’ niitwe mwalimu,” alisema.

Dk Ndalichako alisema udanganyifu mwingine ulionekana katika somo la hisabati, hali iliyothibitisha kuwapo kwa maandalizi ya pamoja ya majibu. Katika shule moja wanafunzi 90 walifanya kosa linalofanana.

Awasifu wasimamizi
Dk Ndalichako aliwamwagia sifa wasimamizi wa mitihani hiyo akisema walitimiza wajibu wao kikamilifu.

Alisema kutokana na umakini wa wasimamizi hao wanafunzi waliokuwa wameficha madaftari sehemu za siri walibainika.

“Kuna mmoja wa kike alikuwa ameficha daftari kwenye sehemu za siri, msimamizi akamwona anahangaika kweli hata kutembea hawezi, akatuma walinzi wa kike kumkagua akakutwa ameficha daftari sehemu za siri,” alisema Ndalichako:

“Kwa hiyo wasimamizi walifanya kazi ya ziada, kumfutia matokeo lazima kuwe na ushahidi wa kutosha. Mfano wanakuta mtu amejiandika kwenye kiganja cha mkono ama kanyagio la mguu, huwezi kukata na kuleta kama ushahidi lakini walitafuta mpigapicha wakapata picha wakaleta kama ushahidi.”

Alisema mitihani yote iliyotungwa ilikuwa ndani ya mihutasari na ilitokana na mambo ambayo wanafunzi hao wangetakiwa wayasome ndani ya miaka minne.

CWT: Mgomo hauhusiki
Rais wa Chama cha Walimu Tanzania(CWT), Gratian Mukoba alisema matokeo hayo ni kitu ambacho kimekuwa kikikua kila siku na kwamba kufeli huko hakuhusiani na mgomo wa walimu wa mwaka jana.

“Matokeo haya ni ‘trend’ ya miaka mingi ila watu walikuwa hawajajipanga kuyapokea kama ya sasa. Ni tatizo lililojitokeza kidogo kidogo hadi lilipofikia sasa,”alisema Mukoba na kuongeza:

“Suala hili lisipotafutiwa ufumbuzi, tutazalisha kizazi kitakachokuja kutulaumu kwa sababu hatukukiandalia mazingira mazuri.”

 Mukoba alisema matokeo hayo yasihusishwe na mgogoro wa walimu kwani wakati mgomo ulipoanza tayari walimu walikuwa wameshafundisha zaidi ya nusu mwaka na wanafunzi wangeweza kufanya mtihani.

“Matokeo mabaya hayahusiani na mgogoro, kwa sababu ulidumu kwa muda mfupi. Hata hivyo, wakati wa mgogoro ilikuwa nusu ya mwaka imeshafundishwa,” alisema Mukoba.
                                                                 CHANZO MWANANCHI

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate