Waziri mkuu wa Tunisia Hamadi Jebali, amejiuzulu baada ya kukosa kuafikia makubaliano kuhusu serikali mpya.
Bwana Jebali,alikuwa anajaribu kuunda serikali mpya kufuatia msukosuko wa kisiasa uliosababishwa na mauaji ya mwanasiasa wa upinzani Chokri Belaid wiki mbili zilizopita.
Mauaji ya mwanasiasa huyo yaliyofanyika Februari sita, yalisababisha maandamano na ghasia pamoja na kujiuzulu kwa maafisa wa serikali.
''Niliapa kuwa ikiwa mpango wangu haungefaulu, ningejiuzulu, na nimefanya hivyo,'' alisema bwana Jebali baada ya kukutana na rais Moncef Marzouki.
Akitaja hatua yake kama jambo la kusikitisha , alisema aliamua kujiuzulu ili kutimiza ahadi yake kwa wananchi wa Tunisia.
"watu wetu wana ndoto fulani, ambazo wanataka wanasiasa kuwatimizia. Laizima tuweze kuwaweka imani watu wetu,'' alisisitiza Jebali.
Na aliongeza kuwa, kukosa kufaulu kwa mpango wangu, haina maana kuwa Tunisia imefeli, au mapinduzi hayakuwa na faida,'' akigusia mapinduzi ya kiraia yaliyofanyika miaka miwili iliyopita ambapo rais wa zamani Zine al-Abidine Ben Ali alipinduliwa. .
No comments:
Post a Comment