FRANK
LAMPARD amefunga bao lake la 199 kwa Chelsea pale timu yake ilipofanya
maangamizi ya 4-0 kwa Brentford katika mchezo wa raundi ya nne ya FA
Cup.
Kiungo
huyo wa England ambaye mkataba wake unaisha majira ya kiangazi, sasa
anakaribia kuvunja rekodi ya Bobby Tambling anayeongoza kwa kufunga
magoli mengi zaidi Chelsea, magoli 202.
Lampard akifunga bao la tatu
Hata
hivyo Lampard, 34 kwa kufunga leo anakuwa amefikisha magoli 26 katika
kombe la FA idadi ambayo haifikiwi na mchezaji mwingine yeyote yule wa
Chelsea ndani ya michuano hiyo.
Lampard alifunga dakika ya 71 wakati huo Chelsea tayari ikiwa mbele kwa mabao mawili ya Juan Mata na Oscar. Bao la nne lilifungwa na nahodha John Terry katika dakika ya 81.
Juan Mata akipiga bao la kwanza
Ocsar akitupia bao la pili
John Terry akishangilia bao lake
Chelsea sasa itaumana na Middlesbrough katika mzunguko wa tano.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Cole, Luiz, Lampard (Bertrand 80), Oscar, Mata (Benayoun 76), Moses (Hazard 65), Ba
Goals: Mata 54, Oscar 68, Lampard 71, Terry 81
Brentford: Moore,
Logan, Craig, Dean, Bidwell, Adeyemi, Diagouraga (Reeves 73), Douglas,
Forshaw (Saunders 78) Donaldson, Trotta (Forrester 56).
No comments:
Post a Comment