MANCHESTER CITY imeimarika kutoka kwenye kipigo cha Southampton na kupenya raundi ya sita ya kombe la FA baada ya kuifumua Leeds 4-0.
Ushindi huo umeweka hai matumaini ya City kumaliza msimu ikiwa na taji mkononi.
City
ilichapwa na Southampton 3-1 katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza na
kujikuta inaachwa nyums kwa pointi 12 na watani wao Manchester United.
Yaya Toure alifunga goli la mapema likiwa ni bao lake la kwanza baada ya kurejea kwenye michuano ya Mataifa ya Afrika kabla ya Sergio Aguero hajafunga bao la pili kwa njia ya penalti.
Kipindi cha pili Aguero na Teves wakaipatia City magoli mengine mawili yaliyohitimisha ushindi wa 4-0.
No comments:
Post a Comment