EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, February 10, 2013

Malecela aunga mkono CHADEMA

WAKATI Bunge likitaja wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kama vinara wa vurugu zilizosababisha kikao cha Bunge kuvunjika wiki iliyopita, mkongwe wa siasa nchini, Samuel Malecela, ameunga mkono msimamo wa wabunge hao na kukiri kwamba walikuwa na haki ya kupiga kelele.
WAZIRI Mkuu mstaafu, John Malecela.
Waziri mstaafu,John Malecela
Malecela ambaye amepata kuwa Waziri Mkuu na Makamu Mwenyekiti wa CCM taifa, alisema ni uonevu kwa Bunge kutaka kuwachukulia hatua kwa madai ya kufanya vurugu.

Akitoa maoni yake kuhusiana na mwenendo wa siasa na uendeshaji wa shughuli za Bunge akiwa nyumbani kwake mjini hapa, Malecela alisema ni haki ya wapinzani kutoa hoja zao na kupiga kelele bungeni kutokana na sheria ya kuwapo kwa vyama vingi.

“Wakati wa uanzishwaji wa vyama vingi, nilikuwa katika mchakato huo na tulijua kuwa hayo ni lazima yawepo, kwa kufanya hivyo inaonesha wazi kuwa ni wakati wa vyama vingi na ndiyo maana wakati mwingine wanafanya mambo ambayo yanalenga kuishinikiza serikali kufanya mambo mbalimbali.

“Ikumbukwe kuwa maana ya kuwapo kwa vyama vingi ni tofauti na kuwapo kwa chama kimoja, kama kingekuwapo chama kimoja ingekuwa sawa na kuchezea mpira chini ya meza, kutokana na kuwapo kwa wabunge wa vyama vingi ndiyo maana tunaona hali hiyo inayotafsiriwa kama fujo,” alisema.
Juzi Bunge liliwataja Mbunge John Mnyika (Ubungo), Joshua Nasari (Arumeru Mashariki), Tundu Lissu (Singida Mashariki) na Mbunge wa Viti Maalumu, Paulina Gekul kwamba ndio vinara wa vurugu bungeni, lakini likashindwa kuwachukulia hatua.

Siri ya ripoti yafichuka
Wakati Malecela akitoa kauli hiyo, siri ya kile kilichotokea wakati wa kikao cha kamati ya kuchunguza vurugu hizo imefichuka.
Habari kutoka ndani ya Kamati ya Maadili, Kinga na Madaraka ya Bunge, ambayo kabla ya kuvunjwa ilikuwa inaongozwa na Brigedia Mstaafu, Hassan Ngwilizi, zilisema kuwa kulikuwa na mvutano mkubwa katika kushughulikia suala hilo na matokeo yaliyotangazwa bungeni yana utata mkubwa.

Vyanzo vyetu vya habari vilisema kuwa mvutano huo ulitokana na namna ambavyo kamati hiyo ilivyofanya kazi ya kubaini wabunge waliohusika kwenye vurugu hizo.
”Kwanza walichukua mikanda iliyorekodiwa na TBC, lakini siku hiyo ilipiga picha za meza ya Spika tu. Picha za kamera za CCTV, zilionesha wabunge wakiwasha vipaza sauti, lakini sauti hazisikiki.

“Hansard ilionesha majina ya wabunge hao wa CHADEMA na cha ajabu hakuna hata mbunge mmoja wa CCM,” kilisema chanzo chetu cha habari.
Kibaya zaidi kamati hiyo haikuwaita wabunge hao kujitetea, lakini ikaamua kuleta majina yao bungeni na kushindwa kuwachukulia hatua.

Februari 4, mwaka huu, Bunge la Kumi likiwa katika kikao chake cha tano majira ya jioni palitokea vurugu kubwa ndani ya Bunge, hali iliyosababisha Naibu Spika, Job Ndugai, kuliahirisha Bunge kwa siku hiyo, zikiwa ni dakika chache tangu lilipoanza.
Kuahirishwa huko kulitokana na vitendo vya wabunge kupiga kelele bungeni huku wakipinga kuwa hoja ya Mbunge wa Ubungo John Mnyika (CHADEMA), ilitaka kuondolewa kwa ubabe.

Wabunge vinara
Miongoni mwa majina ambayo yalitajwa na Ngwilizi kuwa ni ndio vinara wa vurugu hizo ni wabunge wa CHADEMA, John Mnyika (Ubungo), Joshua Nasari (Arumeru Mashariki), Tundu Lissu (Singida Mashariki) na Mbunge wa Viti Maalumu, Paulina Gekul.

Mnyika: Kamati imebabaisha
Akizungumzia uamuzi wa kamati hiyo, John Mnyika, alisema imetoa taarifa ya uchunguzi wa upande mmoja bila kuchunguza na kusikiliza wahusika mbalimbali na kimsingi haijawahoji.
Mnyika alisema kilichofanywa na kamati hiyo ni ubabaishaji, kwa vile kamati ilipewa hadidu rejea tatu; ya kwanza ikiwa ni chanzo cha vurugu, lakini yenyewe ikadai ni tafsiri ya muda uliotumiwa na waziri, jambo ambalo alisema ni uongo.

“ Chanzo ni ubishani kuhusu ukiukwaji wa kanuni uliofanywa na naibu spika wa kumruhusu waziri kwa kutumia kanuni ya 57, 1, c, kuwasilisha mabadiliko ya hoja ya kuingiza maneno ya kuondoa hoja ya msingi, uamuzi ambao ni kinyume cha kanuni ya 57,4 ambayo inakataza kufanya mabadiliko yanayopingana moja kwa moja na ile ya msingi.
“Na kanuni nyingine ya 58,5 inayosema mwenye mamlaka ya kuondoa hoja ni mtoa hoja pekee kwa azimio la Bunge. Maana hata mtoa hoja akishawasilisha hana idhini ya kuondoa bila ridhaa ya Bunge. Nilipowasilisha hoja asubuhi, hata mimi mwenyewe ningetaka kuondoa ilibidi niombe idhini ya Bunge. Hiki ndicho kiini kikuu cha ubishani uliozuka na kimsingi tulitaka kanuni zifuatwe,” alisema Mnyika.
                                                 CHANZO TANZANIA DAIMA

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate