Makamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha wa timu ya Simba, Rahma Al Kharusi
maarufu kama Malkia wa Nyuki akiongea na aliyewahi kuwa kocha wa timu
hiyo, Milovan Cirkovic.
Baada ya kuhaha kwa zaidi ya wiki moja na nusu akitaka kulipwa fedha zake dola 32,000 kutoka kwa uongozi wa Simba, hatimaye ‘zali’ limemuangukia.
Milovan raia wa Serbia, ameahidiwa kulipwa fedha zake na makamu mwenyekiti wa kamati ya fedha, Rahma Al Kharusi maarufu kama Malkia wa Nyuki.
Mwanamama huyo jana alikata mzizi wa fitina na kupitisha kumlipa Milovan kwa fedha zake huku akisema ameamua kuiondolea Simba aibu.
“Simba ina mambo mengi, lakini sasa hakuna kinachoendelea. Leo wanachama wanachanganyikiwa, hawajui wapi pa kushika. Mambo hayaendi vizuri kwenye klabu, huku kocha huyu anadai.
“Sasa anzunguka tu mitaani anasema maneno, kweli anadai haki yake, kwa nini tusimpe. Mimi sipendi ubabaishaji, nitamlipa,” alisema Rahma.
Baada ya mazungumzo ya takribani dakika nne na Rahma aliomba namba za akaunti ya Milovan na kuahidi kumtumia fedha zake ndani ya siku tatu.
Rahma ambaye aliondoka jana nchini kwenda Oman, alisema atatuma fedha hizo kwa Milovana na kumtaka awe na subira hadi atakapotua Oman leo usiku.
Milovan ambaye alikuwa kama ameshangazwa na hali hiyo kwa kuwa kesho alipanga kutua TFF kufikisha mashitaka yake, alisema amefurahishwa sana na Malkia wa Nyuki.
(PICHA/HABARI NA SALEH ALLY / GPL)

No comments:
Post a Comment