L-R: Rais Dk Shein na Askofu Shao (picha na Ramadhan Othman, Ikulu-Zanzibar)
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed
Shein leo ameungana na viongozi wa dini, waumini pamoja na wananchi
wenye mapenzi mema, katika kutoa salamu ya mwisho kwa mwili wa Marehemu
Padre Evaristus Gabriel Mushi, kwenye Kanisa la Minara Miwili Mjini
Zanzibar.
Padre Mushi aliaga dunia kwa kupigwa risasi na watu wasijuilikanwa Jumapili iliyopita wakati akielekea kuongoza misa ya kwanza ya kipindi cha Kwaresma. Mwili wake umepumzishwa leo katika Kanisa la Kitope, Kaskazini B, Unguja.
Padre Mushi alizaliwa tarehe 15 Juni 1957 mkoani Kilimanjaro, akiwa ni mtoto wa nne katika familia ya watoto sita. Alikuwa msomi wa Shahada ya Uzamivu ya Elimu ya Ushauri nasaha aliyoipata nchini Marekani.

No comments:
Post a Comment