Kikosi
cha Young Africans imeendelea na mazoezi katika uwanja wa
Mbegani nje kidogo ya mji wa Bagamoyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya
mchezo wake dhidi ya timu ya Azam Fc siku ya jumamosi katika Uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam.
Young Africans ambayo imeweka kambi katika hoteli ya
Kiromo - Bagamoyo tangu jana mchana kujiandaa na mchezo huo, leo asubuhi
imefanya mazoezi chini ya kocha mkuu Brandts, kocha msaidizi Fred Felix
'Minziro' na kocha wa makipa Razaki Siwa huku wachezaji wote wakiwa
katika hali nzuri kiafya na kiakili kuelekea katika mchezo wa jumamosi.
Kikosi
cha mholanzi Ernest Brandts kinaonekana kuwa kwenye hali nzuri na
wachezaji wote wanaoekana kuwa kwenye ari ya mchezo huo wa jumamosi
kwani mechi hiyo ndio itakayotoa taswira ya msimamo wa Ligi Kuu kuelekea
katika mbio za kutwaa Ubingwa.
Young Africans
ambayo katika mchezo wake wa mwisho iliibuka na ushindi wa jumla ya
mabao 4-0 dhidi ya timu ya African Lyon huku safu ya ushambuliaji wa
timu ya Yanga ikionekana kuwa na uchu wa kucheka na nyavu katika kila
mchezo.
Akiongea na www.youngafricans.co.tz Brandts
amesema kikosi chake kipo katika hali nzuri, mazingira ya kambi ni
mazuri, wachezaji wanapata fursa ya kukaa pamoja na kushiriki mazoezi
kwa pamoja katika hali ya utulivu hali inayongeza umakini katika kuelewa
maelekezo yake.
Najua
macho na masikio ya wapenzi wa soka nchini yansubiri kuona nini
kitatokea siku ya jumamosi, ukweli ni kwamba huo ni mchezo muhimu sana
kwetu ili kujijweka katika hali nzuri ya kuendelea kuongoza ligi , hivyo
nachoweza kusema ni kwamba nimekiandaa kikosi changu ili kiweze kuibuka
na ushindi katika mcheo huo siku ya jumamosi 'alisema Brandst'
Aidha
Brandts alisema anafarijika kuwa na wachezaji wake wote 26 kambini
kujiandaa na mchezo huo wa jumamosi, wachezaji wote wapo safi kiafya,
kiakili na morali ya kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo huo,
hivyo nashukuru kuwa fit kwa kikosi changu chote nitapata fursa ya
kumtumia yoyote kati yao.
Young
Africans inaongoza msimamo wa VPL kwa kuwa na pointi 36 huku ikiwa
imecheza michezo 16, imeshinda jumla ya michezo 11, imetoka sare michezo
mitatu (3) na kupoteza michezo miwili (2) huku ikiwa imefunga jumla ya
mabao 33 na kufungwa mabao 12 tu.
Nafasi
ya pili inashikiliwa na timu ya Azam FC yenye pointi 33 ikiwa na mabao
27 ya kufunga na ikiwa imefungwa mabao 14 ambayo leo inashuka dimba la
chamanzi kucheza na timu ya JKT Ruvu katika muendelezo wa michezo ya
Ligi Kuu ya Vodacom.
No comments:
Post a Comment