Mamia
ya waombolezaji katika mji wa Bredasdorp, jimbo la Western Cape, Afrika
Kusini, wamehudhuria mazishi ya msichana aliyebakwa na gengi.
Msichana
huyo wa miaka 17 alikutikana ametolewa matumbo kwenye eneo la ujenzi
mwisho wa juma lilopita na baadae alifariki hospitalini.
Wanaume watatu wamekamatwa kwa kuhusika na ubakaji na mauaji ya msichana huyo na wanatarajiwa kufikishwa mahakamani juma lijalo.
Shambulio
hilo la kikatili limezusha hasira na maandamano kumtaka Rais Jacob Zuma
achukue hatua kupambana na visa vingi vya ubakaji nchini Afrika Kusini.
Chanzo:BBC Swahili
No comments:
Post a Comment