Jeshi
la Polisi mkoani Mwanza limeingia katika kashfa baada ya askari wake
mmoja wa kituo kidogo cha Igogo kudaiwa kumpiga mahabusu na
kumsababishia kifo.
Askari huyo (jina tunalo), ambaye habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zinadai ametoroka baada ya kubaini ukubwa wa kosa alilofanya, anatuhumiwa kumpiga na kumsababishia kifo Alfred Mallya (29), ambaye alikuwa akifanya kazi kama wakala wa usafiri wa mabasi yanayofanya safari zake kati ya Mwanza na Dar es Salaam.
Hata hivyo, juzi NIPASHE liliwasiliana na Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ernest Mangu, kutaka kujua ukweli wa tukio hilo na kusema hakuwa na taarifa kwa sababu alikuwa ndiyo kwanza alikuwa anarejea akitokea safarini mkoani Dodoma.
“Mimi sina taarifa za tukio hilo kwa sababu nilikuwa safarini, lakini nitafuatilia kesho (jana) kisha nitatoa taarifa rasmi jitihada zaidi za kumtafuta Kamanda Mangu, lakini bado alitoa jibu lile lile kwamba hajapata taarifa na anaendelea kufuatilia.
Hata hivyo, taarifa za uhakika ambazo NIPASHE linazo ni kwamba juzi
mmoja wa maofisa wa waandamizi wa Jeshi hilo mkoani hapa alifanya
mazungumzo na baba mzazi wa marehemu na kuahidi kugharimia usafirishaji
wa maiti. Askari huyo (jina tunalo), ambaye habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zinadai ametoroka baada ya kubaini ukubwa wa kosa alilofanya, anatuhumiwa kumpiga na kumsababishia kifo Alfred Mallya (29), ambaye alikuwa akifanya kazi kama wakala wa usafiri wa mabasi yanayofanya safari zake kati ya Mwanza na Dar es Salaam.
Hata hivyo, juzi NIPASHE liliwasiliana na Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ernest Mangu, kutaka kujua ukweli wa tukio hilo na kusema hakuwa na taarifa kwa sababu alikuwa ndiyo kwanza alikuwa anarejea akitokea safarini mkoani Dodoma.
“Mimi sina taarifa za tukio hilo kwa sababu nilikuwa safarini, lakini nitafuatilia kesho (jana) kisha nitatoa taarifa rasmi jitihada zaidi za kumtafuta Kamanda Mangu, lakini bado alitoa jibu lile lile kwamba hajapata taarifa na anaendelea kufuatilia.
Tukio hilo linadaiwa kutokea Februari 8, mwaka huu katika kituo kidogo cha Polisi cha Igogo.
Taarifa za awali kutoka kwa ndugu wa marehemu pamoja na marafiki wa karibu aliokuwa akifanya nao kazi katika kituo cha Mabasi cha Nyegezi, zinadai kuwa siku hiyo alifika mwanamke mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja ambaye alimkabidhi Alfred kiboksi kilichokuwa na samaki. Kwa mujibu wa mashuhuda hao, Alfred alikabidhiwa samaki hao wenye thamani ya Sh. 30,000 ili awasafirishe kwenda Dar es Salaam kama alivyopewa maelekezo na mwanamke huyo.
Imeelezwa kwamba kesho yake mwanamke huyo alirudi katika ofisi ya Alfred na kumweleza kuwa mzigo aliompatia haujafika, lakini yeye (Alfred) alimsisitiza kuwa aliutuma ila kama umepotea yuko tayari kulipa kulingana na thamani yake.
Imedaiwa kwamba mwanamke huyo alitaka alipwe Sh. 300,000 kama fidia ya samaki hao, lakini Alfred alisema yuko tayari kulipa Sh. 100,000 tu na siyo zaidi ya hapo vinginevyo ni bora apelekwe polisi.
“Kutokana na hali hiyo, mwanamke huyo aliamua kuripoti katika kituo kidogo cha polisi kilichopo stendi ya Nyegezi na Alfred alikamatwa na kuwekwa ndani, na huyo mlalamikaji aliondoka,”alisema mmoja wa mashuhuda. Habari zinasema kuwa kesho yake Alfred alihamishiwa katika kituo kidogo cha polisi Igogo ambako kesi yake ilisimamiwa na askari (jina tunalo).
Licha ya kumhoji, inadaiwa askari huyo alimpiga Alfred kwa kutumia kitu chenye ncha kali na kumsababishia majeraha makubwa sehemu za kichwani na miguuni.
Taarifa zimeendelea kudai kwamba kutokana na kipigo hicho, hali ya Alfred ilikuwa mbaya ndipo askari huyo kwa kushirikiana na wenzake walimtoa mahabusu na kumpeleka katika hospitali ya Butimba na kushonwa nyuzi kadhaa kichwani. Inadaiwa kuwa hali ya Alfred iliendelea kuwa mbaya ndipo madaktari wakashauri apelekwe Hospitali ya Rufaa ya Bugando ambako alifikishwa Februari 10, mwaka huu na kulazwa katika wodi namba 606.
Imeelezwa kuwa baada ya kupata taarifa, baba mzazi wa Alfred, Fred Mallya, alisafiri kutoka Moshi mkoani Kilimanjaro hadi Mwanza kumuona mwanaye.
Akielezea kuhusu tukio hilo, Mallya alisema baada ya kupata taarifa alisafiri na kuwasili Mwanza Februari 12, mwaka huu majira ya usiku na kuwa tayari alikuwa amewasiliana na ndugu yake ambaye aliwasiliana na maofisa wenzake waliopo Jijini Mwanza kwa ajili ya kufanya ufuatiliaji wa karibu kuhusu tukio hilo. Kwa mujibu wa Mallya, hatua hiyo ilisababisha baadhi ya maofisa wa Polisi kwenda Bugando na kushauri Alfred ahamishiwe chumba cha uangalizi maalum (ICU) baada ya hali yake kuendelea kuwa mbaya.
“Baada ya mwanangu kuhamishiwa ICU, ndipo nikaanza kufuatilia tukio zima kuanzia Nyegezi, kituo kidogo cha polisi Igogo na baadaye central (kituo kikuu cha polisi) ambako nilikabidhiwa askari mmoja (anamtaja) ili ashughulikie suala langu,”alisema.
Aliongeza kwamba pamoja na mambo mengine, askari huyo alimkabidhi namba za majalada mawili kuhusiana na kesi ya mwanaye ambazo ni MW/CID/CR/543/2013 na MW/IR/1026/2013.
Aliongeza kuwa katika kufuatilia zaidi, alipata fursa ya kuzungumza na mmoja wa maofisa waandamizi wa Polisi ambaye alimhakikishia kushughulikia suala hilo ikiwa ni pamoja na kumsaka na kumtia mbaroni askari aliyempiga mwanaye ambaye inadaiwa tayari alikuwa ametoroka. “Nimekuwa katika harakati za kufuatilia kesi ya mwanangu nikiwa pamoja na ndugu zangu wa hapa Mwanza, lakini leo (juzi) nilipoenda Bugando kumjulia hali nikakuta mwanangu amefariki dunia,” alisema Mallya.
“Juzi saa 4:10 nilikutana na RPC Ernest Mangu akiwa amewasili kutoka Dodoma akakiri Jeshi la Polisi kuhusika na kifo cha mwanangu na akaahidi kusafirisha maiti kwa ndege hadi KIA, kwa hiyo tunasubiri taarifa zaidi kutoka kwao (polisi) ili baada ya postmortem (uchunguzi wa kidaktari) ndipo tusafiri kwenda kuzika,” alisema.
NIPASHE lilimtafuta Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Dk. Japhet Gilyoma, kuthibitisha tukio hilo, lakini simu yake ya kiganjani ilikuwa ikiita bila kupokelewa.
Hata hivyo, habari kutoka mmoja wa madaktari waliomhudumia Alfred kabla ya kufariki dunia ambaye hakutaka jina lake litajwe kwa sababu si msemaji, alithibitisha kutokea kwa kifo hicho.
Alisema Alfred alifikishwa hospitalini hapo Februari 10, mwaka huu akiwa hoi na fomu namba tatu ya polisi ilionyesha kwamba iliandikwa Februari 9, mwaka huu na alifariki dunia usiku wa kuamkia juzi,”alisema daktari huyo kwa kifupi.
Katika tukio jingine, kijana Godliving Makundi (41), mkazi wa kitongoji cha Mrocha kijiji cha Kwamakundi wilayani Moshi, anayedaiwa kuwa na ugonjwa wa akili, amemuua mama yake mzazi, Julitha Kowero (67), kwa kumkatakata na panga na kutenganisha kiwiliwili chake.
Baada ya kufanya mauaji hayo, wananchi wenye hasira nao walimshambulia kwa silaha za jadi yakiwamo mawe na fimbo na kusababisha kifo chake.
Tukio hilo ambalo lilitokea Februari 18, mwaka huu, katika kitongoji hicho wilayani Moshi, limethibitishwa na viongozi wa kijiji cha Makundi.
Mume na baba wa mama na mtoto aliyeuawa, Godliving Makundi, alisema tukio hilo lilitokea saa 7:00 mchana akiwa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Saa kusimamia mafundi wanaoendelea na ujenzi kanisani hapo.
Makundi alisema ilipofika saa 9:00 wakati akijiandaa kurejea nyumbani kwake, kabla hajafika, ghafla alifuatwa na watoto wa ndugu yake na kumtahadharisha kuwa asifike nyumbani kwa kuwa kijana wake amesababisha mauaji. “Walinieleza nisifike nyumbani kwa kuwa kijana huyo (Godliving) alikuwa bado ameshika panga na anasema bado hajamuua baba yake anamsubiri akishafika amuue…nilikaa kwa muda na walipomzingira na kuanza kumshambulia, ndipo nilifika na kuona mwili wa mke wangu,” alisema.
Alisema baada ya kufika, alikuta mwili wa mke wake (Julitha) pembeni ya jiko na kichanja cha kuhifadhia vyombo huku ukiwa umekatwakatwa sehemu kadhaa za mwili. Alisema kabla ya wananchi kumvamia na kumuua kijana huyo aliyemuua mama yake, awali walimsihi aweke silaha chini alizokuwa amezishika na baada ya kukubali, walimkamata na kuanza kumshambulia hatimaye kusababisha kifo chake.
Makundi alisema kijana huyo alimuua mama yake wakati anatoka kuchukua chombo cha kuwekea chakula na akiwa amejificha, alimvizia na kuanza kumkata kwa panga eneo la nyuma na kuendelea kumkatakata hadi alipotoa shingo yake.
Kijana huyo baada ya kufanya mauaji hayo, aliondoka na kichwa cha mama yake umbali wa mita mbili na kurudi tena kwenye uwanja akisema amemaliza kazi moja bado nyingine ya kumuua baba.
Alisema mwanaye ni wa tatu kuzaliwa kati ya watoto sita, na tangu mwaka 1995 akiwa jijini Dar es Salaam, alitibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Hospitali ya Mirembe na Mawenzi bila mafanikio. Makundi aliongeza kuwa alikuwa akitumia dawa hadi mwaka 1998
ilipoonekana hazimsaidii na ndipo daktari mmoja aliposhauri awe anachomwa sindano kila mwezi katika Zahanati ya Kwakirie na sindano ya mwisho alichomwa Februari 5, mwaka huu.
Akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Ukoo, Betuel Makundi, mmoja wa wajumbe wa Halmashauri ya ukoo wa Makundi, Mwinjilisti Loveland Makundi, alisema alishauri familia zenye watoto au ndugu wenye matatizo ya akili kuchukua tahadhari kila wakati ili kuepusha mauaji kama hayo.
Mwenyekiti wa Kitongoji hicho, Emmanuel Ngowi, alisema kijana huyo anajulikana kuwa ni mgonjwa wa akili.
Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz, hakupatikana kutokana na simu yake ya kiganjani kuita bila mafanikio na alipotafutwa aliyekuwa akikaimu nafasi yake siku chache zilizopita, Ramadhani Ng’anzi, alisema kwa sasa yupo likizo.
Imeandikwa na George Ramadhan, Edwiga Ritte, Mwanza na Salome Kitomari, Moshi.,”alisema Kamanda Mangu.Jana NIPASHE lilifanya
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment