MANCHESTER
United wameondoka uwanja wa Santiago Barnabeu wakiwa na faida ya goli
la ugenini baada ya sare ya 1-1 dhidi ya wenyeji wao Real Madrid.
United
walifanikiwa kutangulia dakika ya 20 kwa bao la kichwa la Danny Welbeck
kufuatia kona ya Wayne Rooney lakini dakika 10 baadae, Cristiano
Ronaldo naye akajibu kwa bao la kichwa.
Welbeck akiifungia United bao
Ronaldo akisawazisha bao usiku wa jana
Ronaldo baada ya kusawazisha bao
Kipa wa United David De Gea alikuwa na kazi ya ziada kwa kuondoa michomo mingi ya Real Madrid.
Dakika
ya 34 Manchester United wakakosa bao la wazi pale Danny Welbeck
aliposhindwa kukunjua vizuri mguu wake kumalizia mpira wa krosi ya Robin
Van Persie.
United
ambao walionekana kama wamedhamiria kulinda matokeo ya sare,
walifunikwa sehemu ya kiungo na kujikuta wakikaribisha mashambulizi
mengi.
Hata
hivyo mashambulizi machache ya United yalionekana ya hatari zaidi na
almanusura yangezaa bao dakika ya 72 na 73 kupitia kwa Robin Van Persie.
Lakini
nafasi tamu zaidi ya United ilikuja katika dakika ya mwisho ya muda wa
nyongeza pale Robin Van Persie alipochukua mpira upande wa kushoto na
kuachia kombora kali liliokolewa kwa ncha za vidole na kipa wa Real
Madrid Diego Lopez na kuwa kona ambayo haikupigwa.
Wakati
Van Persie akienda kupiga kona hiyo mwamuzi alipuliza kipyenga cha
mwisho na kusababisha wachezaji wengi wa United kumzonga.
Ni kama wanasema tuatakutana wiki tatu zijazo
Manchester
United sasa wanapewa nafasi zaidi ya kusonga hatua ya robo fainali
katika mchezo wao wa marudiano wiki 3 zijazo ndani ya uwanja wa Old Trafford.
Katika mechi nyingine Shakhtar Donestsk ilitoka sare ya 2-2 Borossia Ortmund
No comments:
Post a Comment