Siku moja baada ya kung'atuka madarakani kwa viongozi wawili wa
Simba, Zacharia Hanspope na Godfrey Nyange, Kamati ya Utendaji ya klabu
hiyo, imetangaza kulifungulia
Tawi la Mpira Pesa la Magomeni.
Tawi la Mpira Pesa la Magomeni.
Pope, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Kaburu, Makamu Mwenyekiti walitangaza kujiachia ngazi Simba juzi kutokana na sababu mbalimbali.
Akitangaza kulifungulia tawi hilo, ambalo Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage alitangaza kulifungia Novemba 26, mwaka jana, Mwenyekiti wa Muda wa Kikao kilichofikia uamuzi huo, Joseph Itangare alisema kuwa sababu kubwa ni kuleta umoja ndani ya klabu.
"Hatuhitaji tena mpasuko Simba, huu ni wakati wa kushirikiana na kuleta hamasa kwa wachezaji, tunataka kuleta umoja kwa kuwa bado tuko katika mapambano ya kuinusuru timu," alisema Itangare.
Hata hivyo, Aden ambaye ndiye aliyekomalia kufungwa tawi hilo, hakupatikana kwa kuwa yuko nje kwa matibabu.
Kiongozi wa tawi hilo, Masoud Awadh alipotafutwa kuzungumzia, alisema kikubwa ni kuitishwa mkutano mkuu Marchi 17 ili waweze kutoa maoni yao na kama kama tawi limefunguliwa inabidi pia wanachama wao watatu nao wafunguliwe.
"Sasa hivi timu imeyumba, lazima waone umuhimu wetu. Hatuna kinyongo kwa sababu tunafanya kazi kwa maslahi ya timu na siy wachezaji wachache," alisema.
Kundi la mpira pesa lilimfungulia kesi Hamis
Kilomoni baada ya kuwakashifu wanatumiwa na matajiri wa klabu kuihujumu
timu. Kesi hiyo itasomwa Machi.
Katika hatua nyingine Kocha msaidizi wa Simba Jamhuri Kihwelu 'Julio' amewataka wachezaji wake kutojihusisha na mgogoro unaoendelea baina ya viongozi na kupaswa kugeukia Ligi Kuu inayoendelea kwa sasa.
Aidha, nahodha wa timu hiyo, Juma Kaseja na kiungo
Mwinyi Kazimoto wamesema wamesikitishwa na taarifa za kujiuzulu
viongozi hao na kusema walikuwa watu muhimu kwenye klabu.
No comments:
Post a Comment