DIWANI wa Mabira, Christian Songambele (58) CCM, amefikishwa
katika Mahakama ya Wilaya ya Karagwe akikabiliwa na makosa mawili ya
mauaji.
Mbele ya Mlinzi wa Amani, Jane Kalegea, Mwendesha Mashitaka wa
Polisi, Juma Lipwata, alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Machi
13 mwaka huu, majira ya saa 10 jioni katika Kijiji cha Omukagendo.
Mwendesha Mashitaka, alidai kuwa katika kutenda kosa hilo, mshitakiwa
alishirikiana na Datius Dominick (45) na Namara Joseph (43) wote
wakazi wa kijiji hicho.
Mshitakiwa hakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji.
Mshitakiwa amepelekwa rumande na kuunganishwa na wenzake wawili ambao
tayari walikwisha kusomewa mashitaka. Kesi hiyo itatajwa Aprili 18,
mwaka huu.
No comments:
Post a Comment