Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
imeendelea kuwazawadia wateja wake kupitia promosheni ya Amka Millione
na Airtel ambapo wateja wawili washindi wa mwezi Machi wamezawadiwa kila
moja kitita cha shilingi milioni 15 kila mmoja.
Washindi hao ni pamoja na bwana Juma Ibrahim Hamza mwenye umri wa miaka 30 ambaye ni mkazi wa Kawe jijini Dar es Salaam na bwana Adnan Ayub Khan umri wa miaka 25 mfanyabiashara katika mkoa wa Simiyu walijishindia kila mmoja milioni 15.

Mshindi
wa shilingi milioni 15 wa promosheni ya Amka Milionea, Juma Ibrahim
Hamza, ambaye ni fundi uashi akilia kwa furaha na kushindwa kuongea
mara baada ya kutangazwa mshindi wa shilingi milioni 15 kupitia
promosheni ya Amka Millionea. Airtel imewazawadia washindi wawili wa
milioni 15 walioibuka washindi mwezi Machi.
Meneja Uhusiano wa Airtel, Bwana Jackson Mmbando (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi wa shilingi milioni 15 bwana Adnan Ayub Khan mara baada ya kuibuka mshindi wa mwezi wa promosheni ya Amka Millionea. Akishuhudia ni Afisa Masoko wa Airtel, Bi Khalila Mbowe.
Afisa Masoko wa Airtel, Bi Khalila Mbowe (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi wa shilingi milioni 15 bwana Juma Ibrahim Hamza mara baada ya kuibuka mshindi wa mwezi wa promosheni ya Amka Millionea. Akishuhudia ni Meneja Uhusiano wa Airtel, Bwana Jackson Mmbando.

Press Release
FUNDI UASHI AIBUKA MSHINDI WA MAMILIONI YA AIRTEL
-Washindi wa Airtel Amka millionea wakabidhiwa shilingi milioni 15
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
imeendelea kuwazawadia wateja wake kupitia promosheni ya Amka Millione
na Airtel ambapo wateja wawili washindi wa mwezi Machi wamezawadiwa kila
moja kitita cha shilingi milioni 15 kila mmoja.
Washindi hao ni pamoja na bwana Juma Ibrahim Hamza mwenye umri wa miaka 30 ambaye ni mkazi wa Kawe jijini Dar es Salaam na bwana Adnan Ayub Khan umri wa miaka 25 mfanyabiashara katika mkoa wa Simiyu walijishindia kila mmoja milioni 15.
Washindi hao ni pamoja na bwana Juma Ibrahim Hamza mwenye umri wa miaka 30 ambaye ni mkazi wa Kawe jijini Dar es Salaam na bwana Adnan Ayub Khan umri wa miaka 25 mfanyabiashara katika mkoa wa Simiyu walijishindia kila mmoja milioni 15.
Akiongea wakati wa kukabidhi mfano wa hundi kwa washindi
hao, Meneja Uhusiano wa Airtel, bwana Jackson Mmbando alisema, leo tunao
washindi wawili waliojishindia shilingi milioni 15 kila moja katika
droo ya mwisho wa mwezi Machi. Tumeendelea kushuhudia Watanzania na
wateja wetu wakiibuka mamilionea kila siku, kila wiki na kila mwezi
kupitia promosheni hii ya Amka Milionea.
Tunaahidi kuendelea
kuwazawadia wateja wetu huku tukiboresha huduma zetu, na kuwapata huduma
bora zenye gharama nafuu kupitia huduma yetu poa ya Airtel Yatosha
inayomuwezesha mteja kuwasiliana na mitandao mingine ya simu za mkononi
kwa bei poa na kupata vifurushi vya ujumbe mfupi na huduma ya internet
bila kulipia gharama ya ziada. Aliongeza Mmbando
Akizungumza wakati wa makabidhiano, bwana
Juma Ibrahim Hamza, mshindi wa milioni 15 alisema, nashindwa jinsi ya
kuongea lakini nashukuru sana Airtel kwa kuweza kunizawadia shilingi
milioni 15 ambazo kwangu ni kama ndoto. Nategemea kutumia pesa hizi
kujenga nyumba yangu ya kuishi pamoja na familia yangu.
Kwa sasa
ninajishughulisha na shughuli za ufundi wa kujenga tiles katika nyumba
za watu na ninajipatia kipato kidogo ambacho nilijibana na kutumia kiasi
kutuma sms wakati wa promosheni ya Amka Milionea ya Airtel. Kama
kujaribu bahati yangu na leo nashangaa kuibuka mshindi wa mamilioni haya
15, namshukuru sana Mungu kwa kweli! Alisema bwana Ibrahim
Binafsi nachukua fulsa hii kuwaasa
Watanzania kushiriki katika promosheni hizi za Airtel na kwa hakika
wataamka washindi kama mimi hivi leo
Kwa upande wake bwana Adnan Khan
ambaye pia ni mshindi alisema, anawashukuru Airtel kwa kuanzisha
promosheni ya Amka Millionea, na kuahidi kuzitumia pesa zake kuendeleza
na kupanua biashara kwa kuwa hiyo ndio shughuli kubwa anayoifanya.
Promosheni ya Amka Milionea imefika mwisho wake ambapo mpaka sasa wateja zaidi ya1458 na pesa taslimu zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 626 zimezawadiwa kwa washindi walioibuka kutoka katika mikoa mbalimbali nchini.

No comments:
Post a Comment