Na Joseph Shaluwa
STAA wa filamu za Kibongo, Irene Uwoya haachi vituko, safari hii ameibuka na kujisafisha kupitia Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza akidai kuwa yeye na tasnia nzima ya sinema za Kibongo hawana tabia za hovyo bali Magazeti Pendwa ndiyo yanasababisha waonekana hivyo.

Irene Uwoya.
Pamoja na skendo nyingine, Uwoya hivi karibuni alinaswa kwenye mtego
baada ya kuingia kwenye kumi na nane za kamera za mapaparazi wa Global
Publishers akiwa na kinda la muziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul ‘Diamond’
wakiingia katika hoteli moja jijini Dar usiku mnene na kutoka mchana wa
siku iliyofuata.
Irene Uwoya.
Akizungumza hivi karibuni kupitia runinga moja
jijini Dar es Salaam, Uwoya alijitetea kwamba sanaa ya filamu za Kibongo
ni safi na kwamba magazeti ndiyo yanayowaharibia sifa.
“Mfano mimi, kama ningekuwa mchafu ningeitwa na rais wa Burundi
kwenda ikulu? Ameniona mimi ni msafi ndiyo maana aliniita mwaka 2011
kupitia sanaa yangu. Tungekuwa wachafu tusingekubalika hadi na viongozi
wakubwa wa nchi, tatizo ni magazeti,” alisema Uwoya akijibu swali la
mtangazaji wa kipindi hicho, aliyetaka kujua kuhusu madai ya wasanii
kuwa na tabia chafu.
Uwoya ni kama alikuwa akikwepa hoja ya msingi na kuyatupia lawama Magazeti Pendwa kwa kuegemea mgongo wa Rais Nkurunzinza, kwa sababu rekodi za skendo zake zipo na yeye mwenyewe anazijua – Mhariri.
Uwoya ni kama alikuwa akikwepa hoja ya msingi na kuyatupia lawama Magazeti Pendwa kwa kuegemea mgongo wa Rais Nkurunzinza, kwa sababu rekodi za skendo zake zipo na yeye mwenyewe anazijua – Mhariri.
No comments:
Post a Comment