SHINDANO la kumsaka mrembo wa Mkoa wa Singida, Redds Miss Singida 2013 linatarajiwa kufanyika Mei 31 mjini hapa.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini hapa jana,
Mratibu wa Miss Singida, Aunt Borah alisema kuwa maandalizi yote ya
shindano hilo yanaendelea vizuri.
Alisema shindano hilo mwaka huu limeboreshwa ikilinganishwa na ya
miaka ya nyuma na kwamba warembo wanamiminika kuchukua fomu za ushiriki.
Aidha, Aunt Bora alisema warembo nane kutoka Singida Mjini tayari
wameishachukua fomu na baadhi walishajaza na kuzirejesha, pia warembo
watatu kutoka Chuo cha Uhasibu tawi la Singida nao wamechukua fomu za
ushiriki.
“Shindano wa kumsaka mrembo wa Wilaya ya Iramba limeishafanyika na
warembo walioshika nafasi ya kwanza hadi ya tatu, watashiriki shindano
la mkoa… lakini kwa sasa naomba nisitoe majina yao, ila nitafanya hivyo
wakati ukifika,” alisema na kuongeza:
“Nitumie tu nafasi hii kuwaomba warembo zaidi waendelee kujitokeza
kujaza fomu, ili kutengeneza mazingira ya kuwa na ushindani wa kweli
utakaotoa washindi ambao watafanya vizuri mbele ya safari.”
Katika hatua nyingine, Aunt Borah ambaye pia anamiliki saluni maarufu
mjini hapa ya Aunt Borah, alisema kwamba kuna wadau wameonesha nia ya
kuwa wadhamini wa shindano la mwaka huu na bado nafasi ipo kwa wengine
zaidi kujitokeza.
No comments:
Post a Comment