Sherehe
za kukabidhiwa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2012/2013 kwa
Mabingwa wapya Young Africans zimenoga baada ya mabingwa wapya kuichapa
timu ya Simba SC mabao 2 -0 katika mchezo uliofanyika katika dimba la
uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na watazamaji
wapatao elfu 60 huku kituo cha luninga cha Supersport kutoka nchini
Afrika Kusini kikirusha moja moja kwa mchezo huo
Young Africans ambayo ilishatwaa Ubingwa wa VPL kabla hata ya Ligi
kumalizika iliingia uwanjani kwa lengo la kuhakikisha inaiubuka na
ushindi katika mchezo kitu ambacho ndicho kilichotkea kwa watoto wa
Jangwani kwa kuibuka na ushindi huo.
Kikosi cha Young Africans
kiliingia uwanjani kwa kuonyesha kinahitaji ushindi tangu mwanzo wa
mchezo huku washambuliaji wake na nafasi ya kiungo wakiwaatesa wachezaji
wa Simba na kushindwa kuonekana kabisa.
Mshambuliaji wa
kimataifa kutoka nchini Burundi Didier Kavumbagu alikuwa wa kwanza
kuipatia Yanga bao la kwanza dakika ya 4 ya mchezo kwa kiichwa
akimalizika mpira uliopigwa pia na mbuyu Twite kwa kichwa kufuatia kona
iliyopigwa na kiungo Haruna Niyonzima.
Baada ya bao la hilo Yanga
iliendelea kulishambulia lango la Simba kupitia kwa washambuliaji wake
Saimon Msuva, Didier Kavumbagu na Hamis Kiiza na kama si umakini wa
mlinda mlango Juma
Kaseja basi Yanga ingeweza kuibuka na mabao mengi
zaidi.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans ilikua mbele kwa bao 1- 0.
Kipindi
cha pili kilianza kwa kasi huku Simba ikifanya mabadiliko ili kujaribu
angalau kuweza kupata bao la kusawazisha, lakini ukuta wa Yanga ulikuwa
imara kitu ambacho kiliendelea kuwapunguza makali washambuliaji wao.
Dakika
ya 63 Hamis Kiiza aliipatia Yanga bao pili kufuatia mpira uliorushwa na
mlinzi Mbuyu Twite kugusa kwa kichwa na Nadir Haroub 'Cannavaro' kabla
ya kumkuta Hamis Kiiza aliyeukwamisha mpira wavuni na kuhesabu bao la
pili.
Nizar Khalfani aliyechukua nafasi ya Hamis Kiiza nusura
aipatie Yanga bao la tatu dakika ya 88 ya mchezo baada ya mpira wa
adhabu alioupiga kuokolewa na mlinda mlango Juma Kaseja ambaye ilibidi
atibiwe kwa dakika kadhaa kufuatia kupata maumivu.
Dakika ya 89 ya
mchezo mwamuzi Martin Saanya ilibidi atibiwe kufuatia kuishiwa nguvu
ghafla wakati akiamulia kutokuelewana kwa wachezaji Nassoro Masoud
'Chollo' na Didider Kavumbagu, huduma ya kwanza na madaktari walimpa
msaada akaamka kisha kuendelea na pambano.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 2 - 0 Simba SC.
Kikosi cha Yanga:
1.Ally Mustafa 'Barthez', 2.Mbuyu Twite/Juma Abdul, 3.David Luhende,
4.Nadir Haroub 'Cannavaro' (c), 5.Kelvin Yondani, 6.Athumani Idd 'Chuji'
7.Saimon Msuva, 8.Frank Domayo, 9.Didier Kavumbagu, 10.Hamis
Kiiza/Nizar Khalfani, 11.Haruna Niyonzima
Simba :
1.Juma Kaseja, 2.Nassoro Msoud, 3.Haruna Shamte, 4.Mussa Mudde,
5.Shomari Kapombe, 6.Wlilliam Lucian, 7.Mwinyi Kazimoto, 8.Abdallah
Sesseme, 9.Mrisho Ngassa, 10.Amri Kiemba/Jonas Mkude, 11.Haruna
Chanongo/Abdallah Singano
No comments:
Post a Comment