JUMLA ya wanafunzi 7,338 hawakujiunga katika shule mbalimbali za
sekondari za kata wilayani Karagwe, Kagera katika kipindi cha mwaka
2010 hadi 2012.
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Darry Rwegasira alibainisha hayo jana
alipokuwa akiwatuhumu madiwani wa halmashauri hiyo kwenye Ukumbi wa
Rafiki wa Angaza uliopo wilayani hapa.
Alisema wanafunzi hao hawakujiunga na elimu ya sekondari pamoja na kufaulu mtihani wa taifa katika kipindi hicho.
“Tuwaandalie watoto wetu urithi wa elimu kuliko tabia zilizopo za
kuchangia harusi na kuwasahau watoto ambao ndio watakaolikomboa taifa
hili kwa nyanja zote,” alisema Rwegasira.
Alibainisha katika mwaka 2010 wanafunzi waliochaguliwa walikuwa 5,150.
Kati ya hao 1,177 hawakuripoti shuleni, mwaka 2011 wanafunzi 5,107
walichaguliwa na 2,155 hawakuripoti shule na katika mwaka 2012 kati ya
8,871 wanafunzi 4,006 hawakuripoti shuleni.
Hata hivyo, alisema shule nyingi za sekondari katika wilaya hiyo
hazina miundombinu iliyodumu kutokana na baadhi ya wazazi kutokuwa na
mwamko wa kuchangia maendeleo ya shule na kuongeza kuwa kata ambazo
hazina sekondari za kata zimekuwa na tatizo katika kuchangia maendeleo
ya shule za kata zilizo jirani.
No comments:
Post a Comment