Picha
juu na chini ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal akiwasili na kusalimiana na viongozi mbalimbali
wa serikali katika hafla ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Viwanda
katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez,
lililopo eneo la Pongwe nje kidogo ya jiji la Tanga
ambalo linalosimamiwa na Wawekezaji kutoka nchini Korea Kusini akiwa
ameambatana na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bi.Chiku Gallawa.(Picha zote na Zainul Mzige wa Dewji Blog).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal
akiweka saini kitabu cha wageni katika meza kuu. Kushoto ni Waziri wa
Viwanda na Biashara ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Handeni Dk.
Abdallah Kigoda na Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bi. Chiku Gallawa.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiwahutubia wakazi wa jijini Tanga, wakati alipofika eneo la Pongwe
jijini Tanga leo kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa
Viwanda katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez,
ambalo linasimamiwa na Wawekezaji kutoka nchini Korea Kusini.
Baadhi ya wanachi wa jiji la Tanga wakimsikiliza mgeni rasmi Mh. Dk. Mohammed Gharib Bilal wakati akisoma hotuba yake.
Waziri
wa Viwanda na Biashara ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Handeni Mh. Dk.
Abdallah Kigoda akitoa risala yake wakati wa hafla hiyo ambapo
amewaahidi wakazi wa Tanga kufufua viwanda vyote vilivyokufa mkoani
humo.
Mwenyekiti
wa Tanga Economic Corridor Bw. Chris Incheul Chae akizungumza machache
na wakazi wa Tanga na kuwaambia kwamba hawatojutia nafasi waliyowapa
wawekezaji hao kutoka nchini Korea ya Kusini.
Wageni
waalikwa kutoka ndani na nje ya nchi wakati wa hafla ya kuweka jiwe la
msingi eneo la Viwanda lililopo Pongwe nje kidogo ya mji wa Tanga.
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Maeneo Huru ya Uwekezaji (EPZA) Dkt. Adelhelm Meru
akizungumzia mradi huo ambapo ametoa kwa Mkoa wa Tanga kuhakikisha
wanafikisha miundombinu muhimu kama maji na umeme ili wawekezaji wasije
kupata kikwazo wakati wa utekelezaji wa mradi huo.
Naibu
waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ambaye pia ni mwenyeji
wa mkoa wa Tanga Mh. Ummy Mwalimu akitoa salamu kwa wananchi ambapo
amesema wakazi wa Tanga sio wavivu kama fikra za waliowengi na kusema
watachangamkia fursa hiyo kubadilisha maisha yao.
Mbunge
wa Tanga Mjini, Mh. Injinia Omary Nundu (CCM) akizungumza na wananchi
wake na kusema kuwa CCM inatekeleza ilani yake ya kuleta maendeleo kwa
wananchi wake kupitia fursa mbalimbali na kuwataka kutoa ushirkiano kwa
wawekezaji hao.
Aisee
tunashukuru sana kwa kutupa nafasi ya kuwekeza nchini kwako…!
Mwenyekiti wa Tanga Economic Corridor Bw. Chris Incheul Chae
(kulia)akiteta jambo na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maeneo Huru ya
Uwekezaji (EPZA) Dkt. Adelhelm Meru wakati wa hafla hiyo.
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Bi. Chiku Gallawa akitoa nasaha zake kwenye
halfa kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa Viwanda katika eneo maalum la
Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez, lililopo eneo la Pongwe nje
kidogo ya jiji la Tanga ambalo linalosimamiwa na Wawekezaji kutoka
nchini Korea Kusini.
Mgeni
rasmi Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal akirusha mchanga ikiwa
ni ishara ya uzinduzi wa ujenzi wa viwanda hivyo. Wanaoshuhudia tukio
hilo ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bi.Chiku Gallawa (kushoto) na Mwenyekiti
wa Tanga Economic Corridor Bw. Chris Incheul Chae ( wa pili kulia).
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Maeneo Huru ya Uwekezaji (EPZA) Dkt. Adelhelm Meru
(kushoto), Mstahiki Meya wa jiji la Tanga Omary Guledi wakishiriki zoezi
la kurusha mchanga.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akipanda Mti wa kumbukumbu katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga
Economic Corridor Sez, baada ya kuweka rasmi Jiwe la Msingi la ujenzi wa
viwanda katika eneo hilo wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo
jijini Tanga.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akionyeshwa na kupewa maelezo baadhi ya vifaa kama Solar Cooker,
ambavyo ni baadhi ya vitakavyokuwa vikizalishwa katika Viwanda hivyo
baada ya kukamilika, mara baada ya uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa
Viwanda, katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga Economic Corridor Sez,
wakati wa sherehe hizo zilizofanyika leo jijini Tanga.
Mkuu
wa Mkoa wa Tanga Bi.Chiku Gallawa akiserebuka na wanakikundi cha
uhamasishaji mara baada ya mgeni rasmi Makamu wa Rais Dk. Bilal baada ya
kuweka jiwe la msingi.
Naibu
waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ambaye pia ni mwenyeji
wa mkoa wa Tanga Mh. Ummy Mwalimu (wa pili kulia) akijumuika na wamama
wakitanga wakati wakitoa burudani.
Washiriki wa Redd’s Miss Tanga 2013 nao walikuwa nu miongoni mwa wageni wakati wa hafla ya uzinduzi huo.
Baadhi ya viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi wakati wa hafla ya uzinduzi huo.
Wananchi wa jijini Tanga wakiwa wamefurika eneo la Pongwe kushuhudia tukio hilo la kihistoria katika nchi yetu.
Wana CCM wakionyesha nyuso za furaha na matumaini kwa vizazi vyao vitakavyonufaika na ajira kupitia mradio huo.
Mgeni
rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa
wawekezaji kutoka nchini Korea na baadhi ya viongozi wa Serikali.
Mgeni rasmi katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na wawekezaji kutoka nchini Korea.
Mwenyekiti
wa Tanga Economic Corridor Bw. Chris Incheul Chae akimkabidhi
zawadi Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal kwa kumshukuru kubariki ujenzi wa viwanda
hivyo.
Mgeni
rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed
Gharib Bilal akiwapungia wananchi wa Tanga mara baada ya kuweka jiwe la
msingi la ujenzi wa Viwanda katika eneo maalum la Uwekezaji la Tanga
Economic Corridor Sez, lililopo eneo la Pongwe nje kidogo ya jiji la
Tanga. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Gallawa.
Baadhi
ya wakazi wa Tanga wakisoma ramani ya ujenzi wa viwanda hivyo katika
eneo Maalum la Pongwe lilipo nje kidogo ya jiji la Tanga.
Na. Mo Blog Team, Tanga.
Jumla
ya ajira 2000 zinatarajiwa kuzalishwa katika awamu ya kwanza ya mradi
wa ukanda wa viwanda Mkoani Tanga, unaotarajiwa kuanza mwaka huu hadi
mwaka 2015.
Akizingumzia
mradi huo kwenye eneo la Pongwe nje kidogo ya Mji wa Tanga, Waziri wa
Viwanda na Biashara Dkt. Abdallah Kigoda, amesema mradi huo ambao
utatekelezwa na kampuni ya Afrika Future Forum kutoka Korea ya Kusini
utazalisha ajira hizo baada ya kukamilika kwa ujenzi wa viwanda 20.
Kwa
mujibu wa Waziri huyo hadi sasa tayari wawekezaji 17 wameshaonesha nia
ya kuja kuwekeza huku viwanda viwili vinatarajiwa kukamilika ndani ya
mwaka huu.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Tanga Economic Corridor Chris Incheul Chae,
amesema mradi huo unatarajiwa kugharimu dola za Marekani milioni 277.
Chae
amesema viwanda vitakavyokamilika kwa mwaka huu na kuanza kazi mara
moja ni cha vifaa vya ujenzi na kiwanda cha mafuta aina ya petroli
ambayo yatauzwa kwa bei ambayo mtanzania wa kawaida ataimudu.
Katika
kuhakikisha ajira zinatoka humu humu nchini, amesema watachukua
wahitimu kutoka Chuo cha Ufundi Stadi(VETA) na Chuo Kikuu Huria.
Naye
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akizungumzia ujio wa mradi huo,
amesema Serikali itatoa ushirikiano wa karibu katika kutekeleza mradi
huo pamoja na kuwavutia wawekezaji wengine nchini kutimiza azma ya
mapinduzi ya viwanda.
Hata
hivyo amewataka watendaji kuacha tabia ya kuwazungusha wawekezaji
wanapokuja nchini kwa kuweka taratibu zenye urasimu usiokuwa na tija kwa
taifa .
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Maeneo Huru ya Uwekezaji (EPZA) Dkt. Adelhelm Meru,
ametoa wito kwa Mkoa wa Tanga kuhakikisha wanafikisha miundombinu muhimu
kama maji na umeme ili wawekezaji wasije kupata kikwazo wakati wa
utekelezaji wa mradi huo.
No comments:
Post a Comment